Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bashe aibuka tena na LowassaDar es Salaam. Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amesema anaamini Edward Lowassa hakuenguliwa kwa haki na CCM katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho, na kwamba waziri mkuu huyo wa zamani si pekee ambaye amekumbana na uonevu kama huo.

Bashe, ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana akipeperusha bendera ya CCM, pia amesema kashfa zote zinazoikumba Serikali hutengenezewa suluhisho kwa malengo fulani na si kutafuta muafaka wa haki.

Kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Bashe, ambaye alikuwa kambi ya Lowassa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM, alisema ingawa hana uhusiano tena wa kisiasa na kada huyo, anaona tukio lake kuwa ni historia ya kutotendea haki wanachama wengi wa CCM. “Si Lowassa pekee, wako wengi,” alisema Bashe katika mahojiano hayo.

Na Tumaini Msowoya, Mwananchi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top