Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DC abaini ufisadi Tsh milioni 43 ... Awatupa rumande wajumbe kamati ya shule

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Juma Homera amewaweka lumande wajumbe watatu  wa kamati ya ujenzi ya shule ya sekondari ya Mbesa wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kwa ubadhirifu wa shilingi milioni 43 fedha za ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya shule hiyo.

Waliowekwa lumande katika kituo cha polisi cha Tunduru ni Bw.Issa Awadhi ambaye pia ni Katibu wa CCM kata ya Mbesa,Ester Chilijila na Mohamed Tamia huku akiagiza aliyekuwa mkuu wa shule ya sekondari Mbesa mwalimu Raymond Haule Kuletwa Tunduru kujibia tuhuma za ubadhirifu wa fedha hizo.

Hatua hiyo ya mkuu wa wilaya imekuja baada ya wananchi kulalamikia ubadhirifu wa shilingi milioni 43 ambapo mkuu wa wilaya ya Tunduru bw.Homera ametembelea majengo hayo na kujionea hali halisi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini Mheshimiwa Daim Mpakate amesema kuwa kufuatia ubadhirifufu huo wananchi wa Mbesa wamekata tamaa ya kuchangia maendeleo ya shule ya sekondari Mbesa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top