Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Hatima ya dhamana kesi ya Lema kujulikana leo

Wakati Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema (40) akitarajia kujua hatima ya dhamana yake katika Mahakama Kuu leo, kesho yeye na mkewe Neema Lema (33) watapanda kizimbani kwa kesi ya uchochezi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Ijumaa iliyopita Lema alipelekwa Gereza la Kisongo, Arusha baada ya kunyimwa dhamana katika kesi nyingine ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, hatua ambayo imepingwa na chama chake na mawakili wake.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro alisema hawakuridhishwa na pingamizi la dhamana lililowekwa na mawakili wa Serikali kwani tayari Lema alikuwa amepewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi.

 “Tayari tumefanya mazungumzo kuongeza nguvu za mawakili wa chama ambao wataungana na mawakili wa Arusha kudai dhamana leo,” alisema.

Mmoja wa mawakili hao, Shaki Mfinanga alisema leo wanatarajia kuwasilisha maombi ya dhamana ya Lema wakiwa na mawakili wa Chadema.

Kesi ya mkewe
Wakati hayo yakiendelea, kesho Lema na mkewe watakuwa mahakamani mbele ya kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Arusha, Desdery Kamugisha.

Katika kesi hiyo, Hakimu Kamugisha amewapa dhamana washtakiwa hao katika kesi ya kusambaza ujumbe kumkashifu mkuu wa Mkoa Arusha.

Lema anadaiwa kuwa Agosti 20, 2016 akitumia simu namba 076415**47 ambayo imesajiliwa kwa jina la mkewe, alituma ujumbe kwenye namba ya Gambo 0766 75**75 wenye maneno ya uchochezi.

Maneno hayo; “Karibu Tutakudhibiti kama Uarabuni walivyodhibiti Mashoga”yanadaiwa ya uchochezi kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Adhabu, Kifungu cha 118 (a) na Kifungu cha tatu katika sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Katika shtaka jingine, Lema anashtakiwa peke yake, akituhumiwa kivunja Sheria ya Makosa ya Jinai namba 390 kifungu cha 35 kwa kuhamasisha maandamano kinyume cha sheria wakati wa mkakati ulioitwa Ukuta na chama hicho.

Lema alidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti Mosi hadi 26 kwa kusambaza ujumbe kupitia mtandao wa WhatsApp wakati akijua kufanya ni kosa kisheria. Katika kesi hiyo, Lema na mkewe wanatetewa mawakili wanne, John Mallya, James Lyatuu, Reygod Nkya na Mfinanga.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top