Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ashangaza watu






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza na kwa mara ya kwanza umetumia usafiri ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya bombardier Q400 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambapo ndege hiyo pia ilibeba abiria wa kawaida katika safari hiyo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri na baada ya kuwasili mkoani Mwanza amewahimiza wananchi kutumia usafiri wa ndege za ATCL kwa sababu ni wa bei nafuu na usafiri wake ni wa uhakika.

Amesema kwa kutumia ndege ya ACTL imemsaidia kupunguza gharama kubwa ya usafiri kwa kutumia ndege za binafsi za kukodi kwa ajili ya safari za kikazi za ndani ya nchi.

“Ni ndege zetu ni fahari yetu zipo Tanzania ni lazima sisi Watanzania tuzitumie ipasavyo kusafiria ndio maana na mimi leo nimeamua kutumia usafiri wa ATCL kwa sababu ni mzuri na wa uhakika”

Makamu wa Rais amesema amefurahi kusafiri kwa mara ya kwanza na ndege hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na amehimiza viongozi na wananchi kwa ujumla kutumia usafiri wa ndege za ATCL ili kulipa nguvu shirika hilo katika ufanyaji wake wa kazi kwa viwango bora zaidi.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Mwanza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya siasa ambao waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Akiwa mkoani Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku NNE mkoani humo katika  wilaya za Ukerewe,Ilemela,Nyamagana, Misungwi,Kwimba na Magu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top