Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Sakata la Kagera lamuibua Dk. Slaa



Katibu mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ametoa maoni yake kuhusu sakata la serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania kuhusu kutumia pesa za maafa ya kagera kurudishia miundombinu ya umma

Dr slaa kaandika hivii.........

Kwangu Mimi kitendo cha Mkuu wa Nchi kutangaza pale Tinde, Shinyanga kuwa Serikali haitawajengea wahanga " nyumba zao" na pia sasa Bukoba Kagera kuwa Serikali itashughulika na

Ujenzi wa Miundo mbinu na Taasisi za umma kama shule na kadhalika ni kitendo cha ushujaa. Hakuna unafiki wala ulaghai. Serikali inayopenda "cheap popularity" hupenda kufurahisha kilaghai, kumbe haina uwezo, lakini huwajaza matumaini wahanga. Matokeo ni utu wa binadamu kudhalilishwa. Unahitaji kufika tu Kilosa kujionea ninachosema, kwani hakuna lugha ninayoweza kutumia kueleza maisha yanayowapata watu wale zaidi ya 2,500( wakati natembelea 2014)! Ni hali mbaya sana.
Kwa ujasiri wa kutamka kuwa Serikali itagharimia miundo mbinu na Taasisi za umma, wahanga hao hao pia watanufaika, kwani watoto wao angalao watasoma pazuri, na huduma nyingine za jamii ambazo kimsingi ni jukumu la Serikali nazo zitarejeshwa katika hadhi inayostahili au hata bora zaidi. Huu ni ujasiri na uthubutu ambao ni wanasiasa wachache sana wanao.
Aidha, Serikali haikukaa mbali na kutazama tu, yeyote aliyetaka kufisadi, alivhukuliwa hatua pale pale, hata kama ni kwa " kuhisiwa tu" katika hatua hiyo. Uchunguzi wa vyombo husika ndio utakaothibitisha kama kweli walivhofanya au kujaribu kufanya ni makosa au la. Lakini mali nyingi zilizotolewa na wote wenye mapenzi mema hazikuachwa kutapanywa kama ilivyotokea kule Kilosa.
Hivyo, pamoja na kuelewa sentiments za watu mbalimbali, na kuwaonea huruma wahanga, baada ya hatua ya huduma za awali yaani mahema, huduma za vyakula vya kuokoa maisha, huduma za afya, nisingelipenda Kuona Serikali zinatafuta cheap popularity kwa kuwadanganya wananchi kuwa watapata msaada, amvao kimsingi haina uwezo nao.

Mwenye historia, tangu maafa yameanza kutokea nchini kwetu, atuwekee hapa ni wapi na ni lini Serikali imehusika kuwajengea "umma" mkubwa wa maafa nyumba binafsi, ukiaacha misaada cosmetic ya mbao na bati au matofali kadhaa tu amvayo hatawezi kusimamisha hata " stoo" tu ya kuhifadhia vyombo vya ujenzi. Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu, na tukijua hivyo, badala ya kupoteza muda kulalamika tujielekeze kwenye namba hora zaidi ya kuondoa matatizo haya.

Hapa Canada, Katika Jimbo la Alberta, Mji wa McMurray, watu zaidi ya 70,000 walipaswa kuwa "evacuated" ( kuokolewa) kutokana moto uliokuwa unapelekwa kwa mwendo kasi mkubwa na upepo na Hivyo kuangalia za nyumba nyingi. Tulichangishwa ( kwa hiari na Red Cross, shule, Mamlaka za miji na Mitaa kwa njia mbali. Lakini, fedha zote hizo zilienda zilienda kwenye kujenga miundo mbinu, na huduma ya dharura ya muda mfupi kama nilivyoeleza juu. Wananchi waliopoteza nyumba zao walielekezwa kutumia " Insurance" zao( huduma ya Bima ambayo sisi hatuna kwetu- ni vema kuelekeza mijadala kwenye solutions kama hizo zaidi kwa maafa ya mbele). McMarray, maisha karibu yamerejea katika hali ya kawaida chini ya mwaka mmoja, kutokana na hatua hizo za Serikali kujielekeza kwenye miundo mbinu na wananchi kutumia rasilimali zao. Hakubaki miaka zaidi ya 10 kama Kilosa kwa kuwa Wenzetu hawabaki kulalamika, bali hutafuta solution kwa siku zijazo. Tusiendelee kujidanganya kuwa Serikali itafanya kila kitu. Indonesia, wakati wa Tsunami, pajengwa kutokana na Bima, lakini Serikali imejenga Taasisi za Umma, na Miji takriban yote imerudi kwenye hali yake ya awali. Let us be pro active, "it can be done"

Dr. Wilbrod Peter Sala.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top