Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UVCCM DSM yammwagia sifa Rais Magufuli

UMOJA WA VIJANA WA CCM MKOA WA DSM (UVCCM) PRESS RELEASE.

PONGEZI KWA MHE JOHN POMBE MAGUFULI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA NA KUFANYA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KWA KASI YA HALI YA JUU.

Tarehe 5/11/2016 Mhe Rais John Pombe Magufuli ametimiza Mwaka mmoja tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tangu awe Rais kwa kipindi iki cha Mwaka mmoja Mhe Rais amefanya mambo makubwa kwa Taifa letu... Watanzania wengi wamekuwa na Matumaini mapya kwa Taifa ili baada ya kuona utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kwenye Ilani ya CCM yakitekelezwa kwa kasi hakika safari hii tumepata Rais wa Mwendokasi lazima maendeleo yaende kasi.

Tangu achaguliwe kuwa Rais amefanya mambo makuu yafuatayo:-

1. KUFUTA SHEREHE ZA UHURU KWA KUFANYA GWARIDE,,,  NA BADALA YAKE KUITANGAZA SIKU HIYO KUWA SIKU YA USAFI WA MAZINGIRA KWA TAIFA LETU... KISHA KUAGIZA FEDHA HIZO ZA GWARIDE KWENDA KWENYE UPANUZI WA BARABARA YA BAGAMOYO ROAD... KIPANDA CHA MWENGE.

2. KUSIMAMIA NIDHAMU KWA WATENDAJI WA SERIKALI.

3. KUSIMAMIA NIDHAMU YA FEDHA ZA SERIKALI.

4. KUUNDA MAHAKAMA YA MAFISADI NA TAYARI IMESHAANZA KAZI KWA KUWASIMAMISHA WATUHUMIWA KIZIMBANI.

5. KUSIMAMIA JUU YA KUWABAINISHA WAFANYAKAZI HEWA WA SERIKALINI NA WANAFUNZI HEWA MASHULENI.

6. ELIMU BURE KUANZIA DARASA LA KWANZA MPAKA KIDATO CHA NNE.

7. KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA SHULE NA KUSIMAMIA ZOEZI LA UPATIKANAJI WA MADAWATI NCHI NZIMA.

8. KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA HUSUSAN MAMA NA MTOTO KWA KUJENGA MAJENGO MAPYA KILA KONA HAPA NCHI YATAKAYOKUWA YANATOA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO.

9. KUJENGA CHUO KIKUBWA CHA KUTOA WAHITIMU WA UDOKTA TANZANIA.

10. UJENZI WA HOSTEL KUBWA ZA KISASA CHUO KIKUU CHA DSM.

11. KUJENGA NYUMBA NYINGI ZA KUISHI WANANCHI KWA GHARAMA NAFUU... MF -  MAGOMENI KOTA.

12. UJENZI WA BARABARA YA JUU KWA KWA BARABARA YA MANDELA NA NYERERE ROAD ... (TAZARA).

13. KUZIBA MIANYA YA RUSHWA NA KUPAMBANA NA UHARAMIA WA WANYAPORI KWA KUIMARISHA SAFU YA UONGOZI WA TANAPA.

14. KUIMARISHA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NCHINI.

15. UPANUZI WA BARABARA YA MWANZA AIRPORT KWA KUDHIBITI FEDHA ZILIZOKUWA ZITUMIKE KWA SHUGHULI ZA SHEREHE ZA MUUNGANO MWEZI APRIL MWAKA HUU.

16. KUNUNUA NDEGE MBILI ZA KISASA KWA CASH MONEY NA KUTOA ADVANCE KWA NDEGE NYINGINE TATU (3) IKIWEMO BOENG YENYE UWEZO WA KUBEBA ABIRIA MPAKA 260.

17. KUSIMAMIA AZIMIO LA MUDA MREFU WA KUIAMISHA SERIKALI KUAMIA DODOMA NA KWA SASA TAYARI ASILIMIA 40 - 50 WAMESHAAMIA DODOMA AKIWEPO WAZIRI MKUU.

18. KUWAWAJIBISHA VIONGOZI WOTE WANAOONEKANA WANASHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAO.

19. KUINGIA MKATABA NA UGANDA KWA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAFUTA TOKA TANGA MPAKA KAMPALA UGANDA.

20. KUPAMBANA NA WAUZA MADAWA YA KULEVYA,,, UJAMBAZI NA UGAIDI NDANI YA NCHI YETU.

21. KUSIMAMIA UTOAJI WA MIKOPO KWA WATOTO WA MASKINI NA WANYONGE WASIO NA UWEZO WA KUWASOMESHA WATOTO WAO CHUO KIKUU.

22. KUWAPA FURSA YA KIUONGOZI KATIKA NAFASI NYETI NA KUBWA  WALEMAVU WA AINA MBALI MBALI SERIKALINI.. MF. DKT POSSI NA DKT MPANJU.

23. KUZUIA SAFARI ZA NJE YA NCHI ZISIZO NA TIJA KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SERIKALINI.

24. KURUDISHA NA KUIMARISHA UHUSIANO MWEMA NA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI... MF. RWANDA,,, KENYA NA UGANDA... Ikumbukwe turikuwa tuna mgogoro kiasi wa kimahusiano na nchi hizo kipindi kilichopita.

25. KUINGIA MKATABA NA WAKOREA WA UJENZI WA RELI YA KATI KWA KIWANGO CHA HALI YA JUU,,, JAMBO AMBALO LITALAHISISHA USAFIRI WA MAZAO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUFIKA SOKONI KWA GHARAMA NAFUU.

Hakika huu ni Utumishi uliotukuka katika Taifa letu yaani haijapata kutokea ndani ya mwaka mmoja tu kusimamia mambo mengi kiasi iki.

SISI KAMA UMOJA WA VIJANA WA CCM MKOA WA DSM (UVCCM)Tunaamini Mhe Magufuli ni Chagua la Mungu ... ameletwa kuliokoa Taifa letu kama alivyompeleka Nabii Mussa kwenda kuliokoa Taifa la Waisrael.

Aidha UVCCM Mkoa DSM tunampongeza pia Mhe Rais Magufuli kwa kujibu Maswali ya waandishi wwa habari siku ya 4/11/2015 kwa ufasaha na Weredi wa hali ya Juu... Wananchi tumepata faraja na tunaona dira ya Tanzania mpya mbele ya Nyuso zetu HONGERA SANA MHE RAIS NA WATENDAJI WOTE WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO MLIO CHINI YA WAZIRI MKUU MHE MAJALIWA.

Mwisho tutoe Rai kwa wale wote wanaobeza MAFANIKIO HAYA... tunawaambia huo sio Uzalendo na Sisi kama UVCCM Mkoa DSM hatutowavumilia wale wote wanaoleta chokochoko kwa Taifa letu iwe ndani ya DSM au Nje ya DSM tutawafata kokote walipo  kuwashughulikia mara moja.

Taifa ili ni kati ya Mataifa machache yenye AMANI ya Asili kutoka kwa wazee wetu... tulipata UHURU kwa Amani hatupo tayari kuipoteza Amani hii kwa Tamaa ya wachache wenye uchu wa Madaraka.

Tunawaambia wasubiri 2020 kwa sasa waiache Serikali itimize Ilani yetu pendwa ya CCM.

UVCCM Mkoa DSM tunasema watu wote "TUTII SHERIA BILA SHURUTI - KWA MAANA SERIKALI YETU HAIPENDAGI UJINGA 👮🏽"

Sisi kama vijana wa CCM Mkoa wa DSM tunakuahidi Mhe Rais wetu Mpendwa Magufuli hatutokuangusha tutatimiza wajibu wetu kwa kasi ya (BASI LA MWENDOKASI)... HAPA KAZI TUUUUUUUU.

IMETAYARISHWA NA MKUU WA IDARA YA HABARI UVCCM MKOA WA DSM ... MSEMAJI SAADY KHIMJI KATIBU WA UHAMASISHAJI, SERA NA UTAFITI MKOA WA DSM.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top