Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UVCCM Taifa wakutana ... Waja na maazimio haya ....




         VMM/U.80/8/Vol.I/57                                                                                                            24/08/2016

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa imekutana Jumatano tarehe 23/11/2016 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Sadifa Juma Khamis (MCC) (MB) katika ukumbi wa mikutano  Makao Makuu ya UVCCM Dar es Salaam.

Katika kikao hicho cha kawaida pamoja na mambo mengine kimepokea na kujadili agenda kutoka idara nne za UVCCM Taifa hatimae kufanya maamuzi.

Kamati ya Utekelezaji imeridhishwa na juhudi na mikakati inayoendelea  kuelekea Jumuiya  kujitegemea kiuchumi 100% ili kuweza kujiendesha kwa ufanisi na mafanikio ambapo  imeridhia uondoshwaji wa wafanyabiashara wote waliopo eneo la UVCCM   Kinondoni Mwinjuma ili kupisha uvunjaji na hatimaye kuanza kwa  ujenzi wa vitega Uchumi vikubwa katika eneo hilo ambapo wafanyabiashara waliopo  watapewa hati ya siku tisini (90) ili wawe wameondoka katika eneo hilo. Uwekezaji mpya  katika eneo hilo takriban  kwa asilimia 90% utagharimiwa na UVCCM yenyewe.

Kufuatia tathmini iliyofanywa na UVCCM Taifa nchi nzima kwa kutathmini miradi yake  kuanzia ngazi ya Shida hadi Taifa,  kamati ya utekeleza imeamua na kuelekeza kuimarishwa mfumo wa ukusanyaji  mapato wa jumuiya na kusimamia matumizi yake sambamba na kupitia upya mikataba yote ya uwekezaji kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa ili kuepeka mikataba isiyo na tija kwa taasisi

 Kamati ya utekelezaji imejipanga kuongeza uwezo wa taaluma  kwa watendaji wake wote kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu ili kuwajenga zaidi kitaaluma ili kuendana na  kasi ya mabadiliko ya siasa na kiuchumi.

Kamati ya Utekelezaji imeziagiza Wilaya na Mikoa kutambua kuwa mali na Rasilimali za Jumuiya si milki ya mtu au Kiongozi, kila aina ya mali au kitega Uchumi cha Jumuiya, kinahitaji kulindwa, kutunzwa na kuhifadhiwa na wanajumuiya wote hivyo imewakumbusha kuanzia sasa ni lazima kutekeleza  Azimio la “Siasa na Uchumi” kwa vitendo  kwa kuzingatia Uchumi ni Uhai na kipaumbele cha Taasisi yoyote kuweza  kujitegemea, kujiimarisha na hatimae kujiendesha.

Vile vile Kamati ya Utekelezaji imeziagiza ngazi zote zilizopo kwa mujibu wa Kanuni ya Umoja wa Vijana wa CCM kuhakikisha zinajitathimini na kuendeleza miradi iliyopo pia  kufikiria uibuaji wa miradi mipya ambapo sifa moja ya mafanikio kwa walengwa ni  kuanza  kujitathimini jinsi walivyojipanga katika kufanikisha Uchumi wao na kuepuka kuwa tegemezi na omba omba.

Kamati ya Utekelezaji imepokea maandalizi ya awali ya Uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM 2017 Ngazi ya Shina, Tawi, Jimbo, Wilaya, Mkoa na Taifa ambapo Kazi ya kuchapisha kwa wingi  na kusambaza kanuni ya UVCCM, Kanuni ya Maadili ya UVCCM, Kanuni ya Uchaguzi ya UVCCM pamoja na kuandaa miongozo ya Uchaguzi inaendelea vizuri hivyo imewataka vijana kuzisoma na kuzielewa vyema kanuni.

Kamati ya Utekelezaji imeridhishwa na maandalizi hayo ya awali na imeendelea kuwahamasisha Vijana wenye sifa, uzalendo, ukereketwa na  nidhamu ya Chama kujitokeza kwa wingi kuomba kugombea Nafasi za mbali mbali za Uongozi  katika Chama na Jumuiya zake katika Uchaguzi wa 2017.

Kamati ya Utekelezaji imeendelea kuwakumbusha Vijana wote walioonyesha azma ya kuomba nafasi mbali mbali ndani ya Jumuiya, kuwa kutaka Uongozi si jambo baya ila ukiukwaji wa Kanuni na taratibu zake ni tatizo  hivyo harakati za kuchafuana, kutengeneza makundi au tishio la  kuivuruga Jumuiya kwa kisingizio cha uchaguzi mwaka 2017 vitendo hivyo havitafumbiwa macho kwa vile vinaipunguzia kasi ya Utendaji na utekelezaji wa majukumu taasisi  na ifahamike kuwa UVCCM ina  Kanuni zake, Miongozo, taratibu  na Maadili hivyo muda huu ni vyema  kila mmoja akaendelea na  majukumu yake ya msingi kwa vile kila jambo lina wakati wake.

Kamati ya utekeleza imeridhishwa na kasi ya ulipaji  madeni mbali mbali ya wastaafu na kulipia mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambapo jumla ya T.Shs 205, 456, 754/= zimetumika na wakati huo  imeidhinisha matumizi  ya T. Sh  209, 918, 250/= na kuelekeza fedha hizo zitumike kulipia mafao ya watumishi wanaostafu. Hivyo malipo hayo yafanyike haraka iwezekanvyo kwa wastaafu 35 ambao wamefikia muda wa kustaafu ndani ya UVCCM, aidha kamati ya utekelezaji imewashukuru na kuwapongeza watumishi hao kwa mchango mkubwa waliotoa wakati wakiitumikia  jumuiya kwa kipindi chote katika utekelezaji wa majukumu yao ndani ya jumuiya na Chama kwa ujumla.

Kamati ya utekelezaji imepokea taarifa ya uhaba wa madawati katika Mikoa ya Mara, Simiyu, Rukwa, Kigoma, Geita, Dodoma na Mwanza  na imewagiza makatibu wake wa Mikoa na Wilaya  katika mikoa hiyo, kuhakikisha inasimamia kila kata kutengeneza madawati mawili (2) na kuyakabidhi wilayani ikiwa ni jitihada za kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Rais  Mhe Dk John Pombe Magufuli za kuimarisha na kuandaa  mazingira bora ya utoaji  elimu nchini, hivyo kwa mjumuiko  wa kata zilizoko katika wilaya husika UVCCM itakuwa imekusanya madawati 2136.

Kamati ya utekelezaji imepokea taarifa ya zoezi la uchangiaji wa damu  katika mikoa ya   Dodoma , Tabora, Kagera, Katavi, Mwanza na Arusha iliyofanyika katika wiki ya vijana lengo likiwa  kuchangia damu na kuokoa maisha ya watanzania hasa kina mama na watoto ambapo jumla ya unit 1215.5 zilikusanywa katika zoezi hilo lililozinduliwa na Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka mkoani Kagera.
Kamati ya utekelezaji ya utekelezaji imepongeza mikoa na wilaya zote zilizofanikisha zoezi hili na kuitaka mikoa mingine kuendelea na zoezi hilo kwa vile jukumu hilo ni  endelevu kwa kuzingatia UVCCM ni jeshi la Chama hivyo kazi moja kubwa ni kulinda watu wake hususan  katika suala la afya ya binadamu .

Kamati ya Utekelezaji imetoa  baraka zote na kuunga mkono juhudi, dhamira, malengo na shabaha ya Serikali katika kukomesha zama za ukwapuzi na Matumizi ya jasho la wengine kwa faida ya wachache.
Kamati ya Utekelezaji imeishauri Serikali kuendelea kufanya kila linalohitajika kuhakikisha Uchumi wa nchi yetu unajengeka na kuimarika vizuri zaidi ili kuendeleza mapambano dhidi ya adui ujinga, maradhi na  umaskini.

Mwisho Kamati ya Utekelezaji imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka  2015/ 2020 na mafaniko makubwa  huku akionyesha ushujaa wa hali ya juu katika kuwapigania na kuwatetea wananchi wanyonge.



*Chief Silvester Yaredi*

*Kny: KATIBU MKUU UVCCM TAIFA*
*24  November 2016*
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top