Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wanafunzi darasa la tatu hufanya ngono na madereva

WASICHANA wadogo kuanzia darasa la tatu hufanya ngono na madereva wenye magari makubwa yanayoegeshwa katika eneo la Chalinze Nyama Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Kitendo cha wanafunzi hao kujiingiza katika mapenzi, kunasababisha mimba za utotoni kushamiri katika eneo hilo, ambako nusu ya wasichana walioanza darasa la kwanza, hawakuhitimu mwaka huu.

Hayo yalibainika juzi wakati wa utambulisho wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia na kupunguza ndoa za utotoni katika ngazi ya halmashauri Wilaya ya Chamwino.

Mradi huo unatekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Woman Wake Up (Wowap) ambalo hujishughulisha ushawishi na utetezi hasa wanawake na watoto.

Mtendaji wa Kata ya Manchali, Yohana Msigwa alisema mimba za utotoni katika eneo la Chalinze Nyama ni tatizo kubwa.

“Watoto wadogo wa darasa la tatu, nne na kidato cha kwanza ni shida kubwa, wanashiriki ngono na madereva hata wakipata ujauzito hawako tayari kuwataja wahusika kwani wengi wao hawafahamiki kutokana ni watu wa kupita,” alieleza Msigwa.

Mtendaji wa Kijiji cha Msanga, Joshua Ngubesi alisema wakati mwingine wamekuwa wakikamata watuhumiwa wanaowapa mimba watoto wa shule, lakini wanapokwenda polisi wanakosa ushirikiano.

“Mimi ni nimetuma mgambo akakamate mhalifu unapompeleka mtuhumiwa polisi unaulizwa mzazi wa binti yuko wapi, mpaka aje mzazi ndio mtuhumiwa apokewa tunatumia nauli zetu mwisho wa siku unaambiwa huhusiki,” alieleza Ngubesi.

Ofisa wa Polisi Wilaya ya Chamwino ambaye ni Mratibu wa Dawati la Jinsia, Krista Kayombo alisema wazazi wengi wamekuwa hawafikishi polisi kesi za watoto wanapopata ujauzito.

“Mtoto analetwa kituoni baada ya kushindwa kumalizana kifamilia, kinachotakiwa ni kuwa na ushirikiano kinachofunga mtu ni ushahidi,” alieleza Kayombo.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Chamwino, Sophia Swai alisema kama hakuna ushirikishwaji jumuishi jambo hili halitafanikiwa.

Mratibu wa mradi huo, Samora Mnyaonga, alisema wilaya ya Chamwino ni miongoni mwa wilaya zilizoathiriwa na mimba za utotoni.

Alisema mradi huo utatekelezwa katika kata sita za Mpwayungu, Mlowa bwawani, Makang’wa, Msanga, Manchali na Chilonwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top