Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mkuu Majaliwa amcharukia Dk. Mwakyembe ... Ampa siku 7 akajieleze kwake


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amempa siku saba Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Harrison Mwakyembe kutoa maelezo ya kwanini Tanzania haijakamilisha mkataba wa mawakili wa Afrika Mashariki, mkataba ambao unafanya kutambuana katika utendaji wao wa kazi.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo wakati akimuwakilisha Rais Magufuli katika mkutano wa 21 wa mwaka unaojumuisha chama cha wanasheria wa Afrika Mashariki uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
“Nimeshtushwa kidogo na maelezo kwamba mkataba huu unasubiri tu kusainiwa na wanasheria wakuu wa nchi wanachama, ili uanze kufanya kazi katika nchi zote za jumuiya isipokuwa Tanzania. Natumia nafasi hii kukuagiza waziri uniletee taarifa ofisini kwangu ndani ya wiki moja mnieleze ni kwanini mkataba huu hamkukamilisha kwa kuiingiza Tanzania” – Waziri Mkuu Majaliwa
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top