Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya dirisha dogo la usajili wa January halijafunguliwa vilabu kadhaa barani Ulaya tayari vimeanza kuonyesha kuwataka baadhi ya wachezaji flani kutoka vilabu vingine.
● Manchester City wanafikiria kumuuza kipa Joe Hart ambaye yuko kwa mkopo Torino kwa bei ya 'hasara" paundi milioni 10 lakini nje ya timu zinazocheza katika ligi kuu ya England. (Source: Sun Sport)
● Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amezungumzia mpango wa kumhamisha Alexis Sánchez kwenda kuichezea timu hiyo (Source: El Mercurio)
● Mesut Özil anataka mkataba mpya Arsenal kwa sharti moja tu la kulipwa mshahara sawa na Pogba yani paundi 290,000 kwa wiki. (Source: Evening Standard)
● Tottenham wamekamilisha mkataba wa matangazo katika jezi zao ambapo sasa watapata paundi milioni 25 kwa mwaka kuanzia msimu ujao toka kwa kampuni ya Nike. (Source: Daily Mail)
● Nyota wa zamani wa Barcelona Eiður Guðjohnsen amesema yuko tayari kuichezea Chapecoense ya Brazil ambayo wachezaji wake walikufa katika ajali ya ndege wiki iliyopita. (Source: @Eidur22Official)
● Julian Draxler ameweka wazi mpango wake wa kujiunga na klabu yoyote katika ligi kuu ya England mwezi January. (Source: Daily Mail)
● Kocha wa West Brom Tony Pulis ameweka wazi mpango wa kuwasajili kiungo wa Manchester United Morgan Schneiderlin na mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez katika dirisha la usajili n January. (Source:Telegraph)
● Tottenham wanafikiria kuwasajili moja kati ya makipa Joe Hart au Jordan Pickford wa Sunderland kama ikitokea kipa wao Hugo Lloris ataihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu (Source: Sun Sport)
● Everton, Manchester United na Manchester City zote zimeonyesha nia ya kumsajili beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk. (Source: Sunday Mirror)
● Everton, West Bromwich Albion, Watford na Swansea zote zimeonyesha nia ya kumsajili winga wa Manchester United Ashley Young mwenye miaka 31.(Source: ESPN)
● Liverpool watatakiwa kushindana na PSG ili kupata saini ya kiungo Christian Pulisic mwenye miaka 18 toka Borussia Dortmund.
(Source: BILD)
Loading...
Post a Comment