Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mama Mzazi wa Ben Saanane augua ghafla

DAR ES SALAAM: Ni takriban siku 33 zimekatika tangu Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ben Saanane (32), atoweke katika mazingira ya kutatanisha, habari mpya zinasema mama yake mzazi, Renatha Focus Saanane ameugua ghafla ugonjwa wa presha baada ya kusikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa mdogo wa Ben, Erasto Saanane, awali hawakumpa taarifa za ukweli mama yao kutokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu, lakini hivi karibuni alisikia taarifa za kutoweka kwa mwanaye kupitia redio moja iliyokuwa ikipitia magazeti na kumfanya mama mzazi huyo augue.

“Unajua awali mama hatukumwambia kwamba mwanaye hajulikani alipo kutokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu, maana tulisema tukimwambia atapata mshtuko,  lakini hivi karibuni alisikia kupitia vyombo vya habari na hadi sasa (juzi) hali yake siyo nzuri, kiukweli, alipata mshtuko mkubwa.

“Na mpaka sasa, familia hatuna amani, hatuna furaha kwani hatujapata taarifa zozote kuhusu kupotea kwa kaka. Polisi wanaendelea na upelelezi na sisi tunaendelea kuulizia sehemu tofautitofauti, lakini hili jambo linashangaza sana,” alisema Erasto.

Aliongeza kuwa, Jumapili iliyopita baba yake mzazi, Rabiu Saanane alikwenda Moshi, Kilimanjaro kuangalia maiti moja iliyookotwa ikiwa imefungwa kwenye mfuko wa sandarusi kama zile saba zilizookotwa kwenye mifuko kule Ruvu, Pwani na kuzikwa kando ya mto.

Alisema baba yake alikwenda kuangalia kama maiti hiyo inaweza kuwa ya mwanae huyo ambaye habari ya kutoweka kwake imefika hadi kimataifa.

Ben alitoweka Novemba 18, mwaka huu nyumbani kwake Tabata Dampo jijini Dar, ndugu na jamaa zake wanafanya jitihada za kila namna kumtafuta ikiwemo vituo vya polisi, mochwari na hospitali zote kubwa za Jiji la Dar na hata kwenda mkoani Pwani kwenye maiti 7 zilizookotwa lakini bila mafanikio.

Hata hivyo, hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alisema kuwa, maiti saba zilizookotwa katika Mto Ruvu huenda ni za wahamiaji haramu ambao huingia nchini kinyemela.

Jamii imekuwa ikitoa mitazamo tofauti juu ya kupotea kwa Ben ambapo kila mtu anasema sawasawa na anavyoamini, kuona mazingira au kusikia kutoka kwa watu wengine.

DCI AZUNGUMZIA MIILI  YA WATU SABA, SAANANE

Wakati huohuo, Jeshi la polisi limesema kuwa liliamua kuruhusu kuzikwa kwa miili ya watu saba iliyokutwa pembezoni mwa Mto Ruvu, eneo la Makurunge wilayani Bagamoyo kwa sababu miili hiyo ilikuwa imeharibika vibaya na ilikuwa ikitoa harufu, huku mmoja uliopelekwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, ukishindwa kutambuliwa na ndugu zake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), CP Robert Boaz, alisema wameamua kutoa ufafanuzi huo kutokana na kuendelea kusambaa kwa taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuhusu maiti hizo na uamuzi wa kuzizika haraka.

“Kutokana na ukweli kwamba baadhi ya maiti hizo zilikuwa zimeharibika vibaya, iliamuliwa kwamba maiti sita zizikwe katika eneo la tukio,” alisema Kamanda Boazi.

Kuhusu Saanane, Kamanda Boaz alisema Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea na mwananchi yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwake, aziwasilishe kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu nao.

Pia amewataka wananchi kuwa watulivu kuhusu suala hilo wakati wakiendelea na upelelezi wa kina.

Source: Global Publisher
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top