Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Meya Dar apiga marufuku magari kufungwa minyororo

DAR ES SALAAM: Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amepiga marufuku kampuni zinazohusika na suala la kukusanya ushuru wa maegesho ya magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kuacha kufunga minyororo kwenye magari ambayo yanaengeshwa ndani ya muda mfupi, na kuagiza kuwa wanapaswa kusubiri mpaka saa moja ipite, endapo mwenye gari atakuwa hajatokea ndiyo waendelee na taratibu nyingine.

Pia Meya Mwita amewataka wafanyakazi wa kampuni hizo, kuhakikisha muda wote wanavaa sare ili iwe rahisi kuwatambua.Ameongeza kuwa hadi sasa, tayari zimepatikana zaidi ya mashine 850 ambazo kuanzia Januari, 2017 zitaanza kutumika kukusanyia ushuru wa maegesho ya magari, tofauti na sasa ambapo risiti za kawaida zinatumika.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha wanadhibiti mapato yanayopatikana kutokana na maegesho ya magari, ili fedha hizo ziweze kutumika kwa shughuli nyingine na kuboresha miundombinu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top