Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mfahamu Shujaa aliyepewa heshima baada ya kifo chakeTANZIA: BI KHADIJA KAMBA(1922-2016) MWANAMAMA MPIGANIA UHURU TANZANIA

Anaitwa Hadija Bint Kamba, BintI mrefu mweusi mwenye umbo lililosadifu unyamwezi, asili yake ni Tabora ndipo alipotokea Baba yake na Kigoma ndipo wazazi wa Mama yake walipotokea.

Ni kama ilivyo kwa familia ya Sykes, Bint Kamba alitoka katika familia mashuhuri jijini Dar es salaam katika miaka ya 1950s. Aliingia katika harakati za ukombozi akiwa bintI mdogo mwenye malengo tofauti kabisa na yakipekee sana. Pamoja na kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukoloni tena akiuza roho kwani alikuwa ni Bint pekee wa kiafrika aliyeweza kujichanganya na wazungu, hivyo aliweza kupata siri nyingi za wakoloni na kuwasaidia wapigania uhuru wasikamatwe na wakati mwingine wasidhurike. Alifanya kazi hii kwa siri kubwa sana, kiasi kwamba hakuwa akijulikana sana kwa watu hasa wanaharakati..alikuwa mtu mwenye uwezo wa kipekee wa kutunza siri.

Mwaka 1955 akiwa na Bibi Titi na Bint Maftah walishirikiana kuunda Baraza la Wanawake Tanganyika ikiwa ni kikundi ndani ya TANU kilichokuwa kikitoa ushawishi kwa akina mama kuiunga mkono TANU.

Mwaka 1961 wakati wa Uhuru, Bint Kamba alikuwa ni mmoja wa timu iliyoundwa kubuni nembo ya Taifa (maarufu kama nembo ya ikulu ama nembo ya adamu na hawa ambayo mpaka sasa imeendelea kuwa alama kuu ya Taifa {baadhi ya waandishi wanamtaja kuwa yule mwanamke anayeonekana kwenye nembo hiyo ndiye Bint Kamba).

Novemba 2 ya Mwaka 1962 Mwalimu Nyerere alipotangaza kuunda Umoja wa Wanawake wa Tanganyika (UWT) Bint Kamba alikuwa ndio mpanga mikakati na mfumo wa uongozi wa UWT.
Pamoja na kushiriki katika mapambano ya kudai uhuru akiwa msiri mkubwa wa Mwalimu Nyerere, Bint Kamba hakuwahi kushika nafasi yeyote ya kisiasa kwa kugombea ama kuteuliwa. Baada tu ya nchi kupata uhuru Bint Kamba alieleza kuwa LENGO lake limetimia na kwamba haitaji CHEO chochote.

Mwaka 1985 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwalimu Nyerere akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Pamoja na Baraza la Wazee wa Dar es salaam juu ya kung'atuka alimtaja mtu mmoja ambaye ni wa kipekee aliyeyashangaza maisha yake ya uongozi. Alimtaja Hadija Bint Kamba kuwa ni mwanaMAMA na MPAMBANAJI wa kipekee aliyeshiriki mapambano ya uhuru bila tamaa ya cheo. Mwalimu Nyerere alisema kuwa amekaa ikulu kwa miaka 25 na kila alipotaka kumteua, Hadija Bint Kamba aliendelea kubaki na msimamo wake kuwa HAKUPIGANIA CHEO bali alipigania HAKI na USAWA...alitaka kuona Mwafrika anathaminiwa katika nchi yake na kwamba ametimiza LENGO hilo.

Tangu Mwaka huo wa 1985, Mwalimu alimtangaza Bint Kamba kuwa ni Shujaa asiyevaa Nishani, na tangu wakati huo alishirikia vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mikutano Mikuu yote akiwa ni mwalikwa mpaka pale umri ulipokuwa mkubwa na kumfanya ashindwe kuhudhuria vikao na mikutano hiyo.

BIBI HADIJA BINT KAMBA amefariki jana tarehe 30/11/2016 akiwa ni miongoni wa waasisi waliobahatika kuishi kwa muda mrefu katika nchi huru ya TANZANIA.

Bint Kamba amezikwa mchana wa Leo tarehe 1 Desemba 2016 katika makaburi ya Kisutu yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Anakufa bila CHEO lakini anazikwa kwa heshima ya KIONGOZI wa kitaifa, kwa msafara wa Magari ya askari na viongozi wa Chama na Serikali kutoka mtaani kwake mtaa wenye jina lake Bint Kamba street Ilala Bungoni mpaka Kisutu. Maraisi wastaafu, Katibu Mkuu wa Chama, Naibu Katibu mkuu na Viongozi wengine wa Chama wakiongoza jeneza lenye mwili wake.

Anakufa bila UTAJIRI lakini anazikwa kwa HADHI ya Bilionea.
HIVI NDIVYO ULIVYO MWISHO WA WATU WEMA...!!!
PUNZIKA KWA AMANI MAMA...
Copy and paste from  Mzalendo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top