Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Msanii Bongo movies, Ben apata ajali mbaya


Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho,  Ben Branco Selengo amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali mbaya ya gari siku ya sikukuu ya Christmas.

Muigizaji Mboto ambaye ni rafiki wa karibu wa Ben, kupitia instagram ameandika:

Ajali ulioipata sio ndogo kwetu sisi wanadam, lakin kwa mungu ni ndooogo sana. Naamin ndogo kwa mungu kwasababu utapona kwa uwezo wake mungu. Utapona tu inshaallah (Benn Blanco Selengo)

Akiongea na Bongo5 asubuhi hii ndugu wa karibu wa Ben kupitia simu ya Ben, alidai Ben alipata ajali mbaya ya gari juzi na hali yake bado ni mbaya.

“Ben hali yake siyo nzuri kusema kweli,” alisema dada huyo aliyejitambulisha kwa jina na Sarah. “Alipata ajali ya gari juzi na hapa tunapozungumza bado yupo Muhimbili hospitali,”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top