Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli aombwa kuisaidia Sudan

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan Kusini, Rebecca Nyandeng Garang de Mabior, Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

Baada ya mazungumzo hayo, mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan Kusini, Rebecca Mabior alisema yeye na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania kuonana na Dk Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa EAC kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan Kusini, huku wakimuomba ashirikiane na viongozi wenzake wa EAC kuisaidia Sudan Kusini kutafuta suluhisho la mgogoro unaolikabili taifa hilo.

“Tumefarijika kuwa hapa katika Ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dk Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuia ya Afrika ya Mashariki akishirikiana na viongozi wenzake wa jumuia hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia ili Taifa la Sudan Kusini liwe Taifa lenye amani.

“Hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa tunachokitaka ni Amani katika nchi yetu na hiki ndio kilio chetu,” alisema Mama Rebbeca Mabior.

Naye Rais Magufuli amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan Kusini kutafuta njia mwafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa hilo.

“Mama Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi ya Sudan Kusini hivyo, ningezisihi pande zote zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la Sudan Kusini,” alieleza Rais Magufuli kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top