Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali yakanusha kuwepo kwa ugonjwa wa ZIKA nchini

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekanusha uwepo wa taarifa juu ya ugonjwa wa ZIKA hapa nchini.

Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dk. Hamisi Kigwangalla wakitolea ufafanuzi jana mbele ya waandishi wa Habari, walisema wananchi wasiogope na wamewatoa hofu kwani taarifa zilizotolewa awali na kuripotiwa na vyombo vya habari walizonukuu kutoka NIMR hazina ukweli wowote na ni  za kupuuzwa.

Aidha, kwa mujibu wa Kaimu Mkuu kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Afya), Bi. Catherine Sungura katika taarifa ya Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu ilieleza: “Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Zika nchini.

"Kama nilivyoeleza mnamo tarehe 31 Januari 2016, ugonjwa huu bado haujaingia nchini, na leo pia napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa kwa sasa Tanzania haujathibitishwa kuwepo na ugonjwa wa Zika. Utafiti uliofanywa na NIMR, ulikuwa ni utafiti uliofanyika nchini wa kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya zika na chikungunya.

Kwa utaratibu wa kitafiti,  hii ni hatua ya awali tu ya kuangalia ubora na uwezo wa kipimo hicho.Matokeo haya bado yanahitaji kuchunguzwa kwa kina zaidi kupitia vipimo vilivyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani.

Wizara itaendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali mbali ndani na nje ya nchi kuendelea na utafiti na ufuatiliaji wa kitaalamu ili kuzuia ugonjwa huu kuwepo Tanzania.

Ufuatiliaji wa magonjwa ni endelevu katika sekta ya afya na tuna taratibu za utoaji taarifa wa magonjwa ya kuambukiza na hatari kama vile zika, ebola na mengineyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top