NCHI za Tanzania na Kenya wamesaini makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano baina ya nchi hizo, ikiwemo maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za nyumba na maendeleo vijijini,Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), uvuvi, mazingira, usafiri wa majini na nishati na madini.
Lengo ni kuboresha na kuimarisha mahusiano baina ya serikali za nchi hizo na watu wake katika siku zijazo na utekelezaji wake utasaidia kuboresha mazingira ya uwekezaji, kurahisisha ufanyaji biashara na kuongeza fursa za ajira kwa vijana wa nchi hizo na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga huku Kenya ikiwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Balozi Dk Amina Mohamed ambao kila mmoja aliambatana na wataalamu kutoka katika wizara zao.
Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo , Mahiga alisema makubaliano hayo ni matokeo ya ziara ya Rais John Magufuli aliyofanya Oktoba 31 hadi Novemba 1 mwaka huu nchini Kenya kwa pamoja na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta walioagiza kuitishwa kwa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ili kupitia masuala mbalimbali yanayohusu mahusiano ya nchi hizo mbili.
Alisema Mkutano wa tatu wa Tume hiyo, ulifanyika Desemba 1 mpaka 3 mwaka huu kwa wataalamu kutoka sekta mbalimbali katika nchi hizo mbili kukutana na kupendekeza maeneo hayo mapya ya ushirikiano.
Pia wataalamu hao wlaikubaliana kuweka mfumo wa ufuatiliaji wa karibu wa makubaliano hayo, utakaoongozwa na makatibu wkauu a wizara hizo kutoka nchi za Tanzania na Kenya na watakuwa wakikutana kila baada ya miezi sita ili kuhakikisha wanaendana na kasi ya viongozi wan chi hizo na kuleta matunda kwa wananchi wa pande zote.
Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kueleza kuwa Tanzania inamuunga mkono Waziri huyo wa Kenya, anayewania nafasi ya mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika akiwakilisha kanda ya Afrika Mashariki.
Naye,Waziri Amina Mohamed alisema ushirikiano huo, utasaidia katika kuimarisha uchumi baina ya pande zote mbili kwani nchi hizo, zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu tangu waanzilishi wa mataifa yote mawili. Alisisitiza kuwa utekelezaji wa makubaliano hayo utafanyika kwa wakati.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Duniani Leo1 hour ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment