Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tume ya uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya ubunge, udiwani

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetupilia mbali mapingamizi za wagombea ubunge na udiwani huku ikipokea barua za kujiondoa katika kinyang’anyiro cha ngazi ya udiwani za wagombea wa vyama vya ACT-Wazalendo na Chadema.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Hamid Hamid kwa vyombo vya habari, tume hiyo ilipokea rufaa moja ya kupinga uteuzi wa mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar.

Rufaa hiyo ilikatwa na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juma Ali Juma aliyekuwa akipinga maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo kumthibitisha mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdulrazak Khatib Ramadhani kuwa mgombea halali.

Rufaa hiyo ya mgombea wa CCM ilikuwa na sababu mbili ambazo ni mgombea huyo wa CUF kutorudisha fomu za uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria na hakudhaminiwa na chama cha siasa kugombea ubunge.

“Katika kikao, tume imepitia rufaa hiyo na kuona sababu zilizotolewa na mkata rufaa hazina nguvu ya kisheria, kwa kuwa mgombea wa CUF amerudisha fomu za uteuzi kwa mujibu wa sheria na taratibu,” ilieleza taarifa hiyo.

Aidha, ilieleza kuwa fomu za mgombea huyo wa CUF zimesainiwa na kugongwa muhuri wa Katibu wa Wilaya ya Magharibi B, hivyo tume hiyo imekubaliana na uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo kuwa mgombea huyo amekidhi vigezo na uteuzi wake ni halali.

Katika hatua nyingine, tume hiyo imetoa maamuzi ya rufaa tatu zilizowasilishwa na wagombea udiwa wa Kata za Kijichi (Dar es Salaam), Misugusugu (Kibaha), na Ihumwa mkoani Dodoma.

Katika kata ya Misugusugu, ilikuwa ni ya mgombea wa Chadema, Gasper Ndakidemi dhidi ya mgombea wa CCM, Bogasi Ramadhani na katika kata ya Kijichi, rufaa ilikuwa ni ya mgombea wa CUF, Khadija Shamas dhidi ya mgombea wa Chadema, Fredrick Rugaimukamu.

Kwa Kata ya Ihumwa, rufaa ilikuwa ni ya mgombea wa Chadema, Magawa Juma dhidi ya maamuzi ya msimamizi wa uchaguzi. Tume hiyo ilipitia rufaa hizo na kuzitupilia mbali rufaa za Ndakidemi na Khadija kwa kuwa hazina mashiko.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kuhusu rufaa ya Juma mgombea wa kata ya Ihumwa, tume hiyo ilipokea barua ya msimamizi uchaguzi, Manispaa ya Dodoma, ikiwa imeambatishwa na barua ya mgombea huyo kuiondoa rufaa yake na kwamba anakubaliana na maamuzi ya msimamizi huyo ambayo yalimuengua.

“Tume imepokea barua za kujitoa kwa wagombea wa Chadema na ACT - Wazalendo katika Kata ya Ihumwa. Kwa maana hiyo Rufaa iliyokuwa imekatwa na mgombea wa Chadema, Kata ya Ihumwa imeondolewa kwa kuwa mkata rufaa ameiondoa na amejitoa kugombea kabla haijasikilizwa,” ilieleza.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top