Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva (katikati), ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia wakati akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Temeke viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva (Wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maonesho wa maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Temeke katika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha akihutubia kwenye uzinduzi huo.
viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau na wananchi wakifuatilia hutuba za mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva.
Maofisa Wanawake wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia wakiwa kwenye Maonyesho hayo.
Wananchi na wadau wengine wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi
Wananchi na wadau wengine wakiwa kwenye maonyesho hayo.
Hapa ni kazi tu.
Mrakibu wa Jeshi la Polisi, (SP), Faidha Suleiman (kushoto), ambaye anashughulikia dawati la jinsia Makao Makuu ya jeshi hilo akimkabidhi Mgeni rasmi DC wa Temeke machapisho mbalimbali ya ukatili wa kijinsia ikiwemo miongozo ya uanzishaji wa dawati la jinsia na watoto ndani ya jeshi hilo.
Mrakibu wa Jeshi la Polisi, (SP), Faidha Suleiman (kushoto), akimuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Temeke kuhusu kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo kwenye idara ya dawati la jinsia.
Wananchi wakipata machapisho mbalimbali.
Na Dotto Mwaibale
WANANDOA wanaojimwa ujumba na wenza wao wametakiwa kwenda kushitaki dawati la jinsia yaliyopo vituo mbalimbali vya polisi ili kupatiwa utatuzi wa changamoto hiyo.
Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva wakati akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na watoto katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo ambayo yalishirikisha wadau mbalimbali kutoka Hospitali ya Amana wilayani Ilala na wananchi.
"Ukatili wa kijinsia si kupigana na kutukana hata mume na mke wakinyimana unyumba pia ni ukatili wa kijinsia hivyo anayejimwa hasione aibu aende kushitaki dawati la jinsia katika kituo chochote cha polisi" alisema Lyaniva.
Lyaniva aliwataka wananchi wanao fanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenda kwenye dawati hilo kupata ushauri kutoka kwa maofisa wa polisi waliopatiwa mafunzo ya kutatua changamoto hiyo.
Katika hatua nyingine Lyaniva aliwaagiza maofisa wa polisi wa dawati hilo kutotoa nje siri za watu wanaopeleka malalamiko yao katika dawati hilo kwa kufanya hivyo ni kukiuka utaratibu wa kazi.
Aliwaasa wanandoa kuwa na mshikamano na upendo ili kuwa na familia bora na yenye maadili jambo litakalosaidia kutokuwepo kwa watoto waliokosa maadili na kujiingiza kwenye makundi ya kiovu kama panya road.
Lyaniva aliwaomba wanawake pale wanapopata mafanikio ya maisha kupata fedha au kupanda vyeo kuacha kuwadharau waume zao ili kuepusha kuvinjika kwa ndoa zao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto amewataka wananchi wasiogope kwenda kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia katika vituo vya polisi kwani malalamiko yao yatasikilizwa kwa faragha na maofisa maalumu wa jeshi hilo.
Maonyesho hayo yamedhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN).
Post a Comment