Wakati bei ya korosho ikifikia hadi shilingi elfu nne kwa kilo moja ya korosho ghafi, chama kikuu cha ushirika cha Tandahimba na Newala TANECU ambacho kimefikia bei hiyo kimekusudia hadi kufikia sikukuu ya krismas kiwe kimemaliza kuwalipa wakulima wake na kuuza jumla ya tani elfu sabini na tano
Hadi kufikia mnada wa nane wa chama kikuu cha TANECU jumla ya tani elfu 67 zimeuzwa huku malipo yakielezwa kuwa baada ya changamoto cha ukosefu wa fedha katika mabenk kumalizika,wakulima watakuwa wamelipwa fedha zao zote na kufukia lengo la kuuza tani elfu 75 kwa wilaya mbili za tandahimba na newala kabla ya sikukuu ya krismas.
Mnada wa nane uliouza korosho zaidi ya tani elfu nane,tani 25 zimeuzwa kwa bei ya juu ya shilingi efu nne,huku kiasi kilichobaki kimeuzwa kwa bei kati ya 3200 hadi shilingi 300.
Loading...
Post a Comment