Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Watu 9 wafariki, 18 wajeruhiwa ajali ya Lori na Hiace

Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugonga gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Amina Masenza alisema dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace hiyo iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara. 

“Lori limeharibika kabisa na Hiace pia imeharibika kabisa,” alisema Kamanda Masenza. 

“Lori hilo liliposhindwa kufunga breki liliigonga Hiace ambalo lilikuwa na abiria na kwenda mbele na kisha kugonga watembea kwa miguu,,” 

Kamanda Masenza alisema katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni, madereva wa magari hayo wote wamejeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi wengine. 

“Dereva mmoja yupo chumba cha upasuaji kwa kuwa mguu wake umevunjika na mwingine yupo wodini,” alisema 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top