Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri ataka Wafanyakazi wasimamishwe kazi

Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Angellah Kairuki amemuamuru mkurugenzi mkuu wa mfuko wa maendeleo ya jamii ya kunusuru kaya masikini kuwasimamisha kazi wafanyakazi 111 wa mfuko huo nchi nzima kwa kushindwa kusimamia ipasavyo nafasi zao na kusababisha baadhi ya watu wasio walengwa kunufaika na fedha hizo kinyume na malengo ya serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi na utawala bora Angelah Kairuki amesema licha ya matokeo ya uhakiki kufanyika kwa umakini na kuondolewa kwa kaya 55,692 zilizokuwa zinajinufaisha na mfuko wa maendeleo kwa jamii wakati si walengwa, amemuamuru mkurugenzi mkuu wa TASAF kuwasimamisha kazi mara moja maafisa watano walioko makao makuu wanaosimamia mpango huu akiwemo mkurugenzi wa uratibu ambao ndio viongozi wasimamizi wakuu pamoja na maafisa washauri na ufuatiliaji 106 walioko kwenye halmashauri walioshindwa kufuatilia na kusimamia mpango huu na kusabaisha hasara ya kulipwa watu wasiostahili.

Licha ya waziri huyo kuakikishia wanahabari kuwa uhakiki umefanyika kwa umakini na kuanzia January mwaka 2014 hadi Septemba mwaka huu zaidi ya bilioni 6 milioni 427 kimeokolewa.

Aidha TASAF makao makuu wametakiwa kushirikiana na halmashauri kuakikisha wanaonufaika na fedha hizo ni walengwa tu na si vinginevyo ambapo baadhi ya wananchi wameonyesha kupongeza hatua ya serikali kuamua kulivalia njuga suala hilo kwani kuna baadhi ya watu waliokuwa wakijinufaisha na TASAF wakati si walengwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top