Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Lema amponza Mwanafunzi chuoni

Mwanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam (ARU) amefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa What’sApp.

Akimsomea hati ya mashtaka, mshtakiwa huyo, Wakili wa Serikali, Adolf Mkini mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa alidai kuwa mshtakiwa huyo  ambaye pia anadaiwa kuwa ni kada wa Chadema Januari 3, 2017
alichapisha taarifa za uongo.

Alidai kuwa mshtakiwa huyo kupitia mtandao wa WhatsApp kwenye kundi linalotumia jina la Lowassa Foundation and Bunge Live alichapisha taarifa za uongo kuwa; Nimepata rehema ya mipango michafu sana iliyokuwa inapangwa na bado inapangwa dhidi ya uhai wa (Mb), Godbless Lema…’

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana kuhusika na kosa hilo.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hana pingamizi na dhamana.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa alimpa masharti ya dhamana mshtakiwa huyo ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh 2 milioni  kwa kila mmoja pamoja na barua.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo aliepuka kwenda lumande baada ya kutimiza masharti hayo ya dhamana.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top