Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Maalim Seif apasua jipu wakati akihojiwa leo

Leo January 29 2017 kupitia Funguka ya AzamTV, katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amehojiwa na kuzungumzia ishu mbalimbali ikiwemo za Profesa Lipumba, Zanzibar na maamuzi yake mengine.

Kweli Lipumba alijiuzulu na alipoonyesha nia ya kujiuzulu tulimfuata kwenda kumuomba sana asiondoke hasa wakati ule tulikuwa tunakabiliwa na uchaguzi lakini akaendelea na msimamo wake, hakufukuzwa

Lipumba kajiuzulu mwenyewe, amekaa baada ya miezi 10 anaandika barua kwamba anatengua jambo hili mimi sijawahi kuliona hilo Duniani

Fedha za ruzuku zimekwenda kwenye akaunti ambayo bodi ya wadhamini, katibu mkuu hawaijui

Ukiingia kwenye siasa lazima ukubali kutukanwa, kushambuliwa, kufungwa hata kifo, mimi yote nimeshapitia isipokuwa kifo-Maalim Seif.

Jimbo la Dimani kihistoria ni la CCM na sisi tuliingia kwenye uchaguzi tukijua tuna kazi kubwa’Ulikosa?

Natarajia muda mfupi ujao nitakuwa Rais wa Zanzibar’

Baada ya kuacha wadhifa safari zote za nje najilipia mwenyewe na siombi serikalini ingawa nina haki
Hakuna namna yoyote Zanzibar lazima vyama vishirikiane, hii itawaleta Wazanzibar pamoja

Haiwezekani chama kimoja cha upinzani kuishinda CCM lakini UKAWA itasaidia

Jecha alisema anafuta uchaguzi ametumia kifungu gani cha katiba, kama nilifanya kosa kutangaza matokeo kwa nini hawakunipeleka mahakamani?

Lipumba alidhani akijiuzulu wengi watamfuata lakini haikuleta athari CUF, uchaguzi 2015 tulishinda majimbo 10 TZ bara,

Mtu akijiuzulu atumpi tena nafasi, katiba yetu hairuhusu hivyo, Mtu anajiuzulu halafu anarudi unafikiri anarudi kwa mema

Siwezi kukiacha chama cha CUF wala sijafikiria kuunda chama kingine.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top