SPIKA wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema mafunzo kwa wabunge ili waweze kusoma vyema taarifa za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) yanahitajika na wataendelea kuyatoa ili kuwawezesha wabunge kuwa na tafsiri sahihi ya taarifa hizo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake, Spika Ndugai alisema kwamba wabunge wengi wanahitaji mafunzo hayo kwa kuwa hawa usuli wa hesabu.
Alisema zaidi ya asilimia 70 ya wabunge ni wapya kwa hiyo suala la mafunzo ni la lazima na tayari walishawafanyia mafunzo kwa kuwa mafunzo hayo hutolewa kwa kila bunge.
Juzi wakati wa mafunzo ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ambapo mada kuu ilikuwa uhusiano kati ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), PAC na LAAC katika kuimarisha uwajibikaji sekta ya umma.
Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Athuman Mbuttuka alisema kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya wabunge kuelewa kilichoandikwa kwenye ripoti ya CAG kutokana na lugha inayotumika kuhusisha maneno ya kitaalamu.
Kutokana na changamoto hizo alitaka mafunzo kuendelea kutolewa ili wabunge waweze kufuatilia ripoti ya kuwajibisha serikali kwa kadiri inavyotakiwa na wala si kutumia kwa ushabiki wa kisiasa. “Wakati mwingine Kamati za Bunge hutumia ripoti ya CAG katika kujijenga kisiasa badala ya kuimarisha uwajibikaji,” alisema Naibu CAG huyo.
Ndugai alisema hata hivyo pamoja na kuwafunza wabunge hao miaka mitano ikiisha wengi hubadilika na hivyo kamati nazo hubadilika ingawa uhalisia wa taarifa hubaki ili wajumbe wapya waweze kuendelea pale walipoachia wenzao.
Akizungumzia hoja za mabadiliko ya mara kwa mara, Spika Ndugai alisema mabadiliko katika kamati hizo zanye wajumbe 30 hufanyika kwa mujibu wa kanuni na kwa maoni yake yeye hazijabadilishwa mara kwa mara.
“Inapotakiwa kubadilisha wajumbe kutokana na sababu za kimsingi hufanyika lakini kanuni zinataka wajumbe wake miaka miwili na mara nyingi kamati hizo hutakiwa kumaliza miaka mitano. “Lakini wakati mwingine hutokea ulazima, unapoambiwa mjumbe mmoja anapita hapa na pale kinyume cha utaratibu hapa unatakiwa kubadili ...” alisema Spika Ndugai.
Katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Abdalah Chikota alisema Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa akibadilisha kamati kila baada ya miaka miwili lakini kwa mapendekezo yaliyofanywa na Bunge la Afrika Mashariki angalau wajumbe wa kamati wawe hata kwa miaka mitano kwani watakuwa na uwezo mpana wa kuhoji.
Spika Ndugai katika mazungumzo yake alisisitiza kwamba hakuna mabadiliko ya kamati na yakiyokea ni yale madogo ambayo hayana athari.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
-
-
Jioni22 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment