Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Polepole apasua jipu la kudhoofu kwa upinzani nchini



*ALICHOKISEMA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA NDG H POLEPOLE KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI TRH 24/01/2017, KUENDELEA KUIMARIKA KWA CCM NA KUDHOOFU KWA UPINZANI*

Leo Ndg H Polepole amezungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano, Lumumba. Amejikita zaidi katika kuelezea mwendelezo wa CCM  kuimarika zaidi na kukubalika na wananchi zaidi huku upinzani ukiendelea kudhoofika kwa kasi kubwa zaidi.
Katika uchaguzi mdogo uliofanyika trh 22/10/2017 ambapo ulihusu jimbo moja la Dimani-Zanzibar na kata 20 Tanzania bara, katika viti vyote hivyo CCM imeshinda jimbo la Dimani na kata 19 kati ya kata zote 20. Hii ni ishara tosha kuendelea kukubalika kwa Chama tawala huku wananchi wakiupuuza upinzani na porojo zao zote. Zifuatazo ni nukuu za Ndg H Polepole;
"Ndg wanahabari ni desturi yetu kuwashirikisha lolote pale ambapo tuna jambo ili wananchi wapate kupitia kwenu"
"Tunasema asante sana wananchi kwa kuendelea kuiamini Ccm"
"Tulikua na chaguzi ndogo kwa nafasi za ubunge&udiwani, tulifanya kampeni nzuri zaidi ktk mambo ya maendeleo"
"Tuliendelea kuwaambia watu juu ya maswala na uelekeo wa Ccm na serikali yake kuijenga Tanzania"
"Licha na hujuma na kubeza sana kulikofanywa na vyama visivyo vya Ccm,bado wananchi mmetupa ushindi mkubwa Ccm"
"Kwa upande wa jimbo la Dimani tumeshinda kwa 78.74% dhidi ya vyama vingine, Ahsante Dimani"
"CUF imepata anguko kubwa sana Dimani hasa ukiangalia takwimu za 2015 na za 2016. Kwetu Ccm tumeinuka sana"
"Ccm imeshinda kata 19 kati ya 20, Ahsanteni sana watanzania kwa imani hii kubwa"
"Shughuli za maendeleo tunazozifanya zitatupeleka katika uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2020"
"Siri ya ushindi huu ni MAGEUZI MAKUBWA YANAYOFANYIKA NDANI YA CCM kwa kauli moja"
"Watanzania tuendelee kuiunga Ccm wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kujerea ktk misingi yabkuasisiwa Ccm"
"Siri nyingine ya ushindi ni KAZI NZURI YA RAIS WA JMT, amefanya kazi kubwa ya kutekeleza matakwa ya wananchi"
"Dhamira ya serikali ya kupiga vita RUSHWA, UFISADI, UBADHILIFU na kuwa na uwakilishi madhubuti"
"Tunaendelea kuikumbusha serikali iendelee kusimamia 10% ya mapato ya Serikali za Mitaa kwaajili ya vijana na wanawake"
"Viwanda vitakuja pale ambapo tutavilinda viwanda vya ndani kwa kutumia vyetu"
"Nchi iendelee inahitaji serikali inayojituma na tumeona serikali ikijitahidi zaidi na zaidi"
"Ccm na viongozi wote watenge muda kuwasikilza wananchi wao, hili tunalisisitiza sana"
"Kuelekea 2020 Ccm tunauona mwanga Mkubwa sana kupitia uchaguzi mdogo na kazi nzuri za serikali yetu"
"Mwisho, mwelekeo wetu ni Mageuzi makubwa katika Ccm ili kiweze kutenda ipasavyo"
"Mwaka huu ni wa Uchaguzi wa ndani basi wanachama tuwalipe wananchi kwa uongozi adilifu, wakujituma"
CCM kama chama chenye Dira na Dhamira ya kweli kuwatumikia watanzania tutaendelea kuhakikisha kuwa Chenyewe pamoja na Seikali yake itajikita katika kuwasikiliza nwananchi na kutatua kero zao kwa wakati na kwa haraka zaidi. Watanzania sasa waone sababu ya wao kujiunga na chama hiki pamoja na kukiunga mkono, CCM ni Chama bora zaidi kuwahi kutokea na hakuna chenye kukifikia kwa ubora, mfumo na taratibu za undeshaji.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top