Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali kuja na pedi mpya zitakazotumika zaidi ya mara mbili

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla amesema serikali inafanya tafiti mbalimbali ili kubaini na kuona kama kunauwezekano wa kupata taulo za hedhi (pedi) ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.

Alisema hayo jana katika mahojianio na EATV kuhusu jitihada za serikali za kuhakikisha afya ya watoto wa kike inalindwa na kuepusha utoro mashuleni kutokana na tatizo la hedhi isiyo salama hasa maeneo ya vijijini na wale wasio na uwezo wa kuzipata taulo hizo.

“Sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kuangalia zile pedi ambazo vijana wanaweza kutumia mwenzi mmoja, miwili hata mwaka mzima, hata kwa miaka miwili,” alisema Kigwangalla. “Kuna nchi mbalimbali wameingiza kwenye soko bidhaa na namna hiyo kwa hiyo na sisi tunaendelea kuangalia tafiti mbalimbali kuhusu usalama wa hizi pedi ambazo unaweza kuzitumia kwa muda mrefu,”

Aliongeza, “Kwa hiyo tunaangalia kama na sisi tunaweza kuziruhusu kuingia nchini na sisi tuziingize sokoni. Lengo letu ni kuangalia usalama kwanza kabla hatujaziruhusu kutumika,”

Amesema serikali inahimiza wazazi na walezi wa watoto wa kike wanapoona mabadiliko yametokea kwa mabinti zao wawafundishe namna ya kujitunza kwa kutumia vifaa ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi sambamba na kuwapa elimu zaidi ili wawe wasafi na kujiepusha na magonjwa yakuambukizwa.

Kwa upande wake mbunifu wa taulo za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja Bi.Jennifer Shigoli amesema katika maeneo mbalimbali waliopitia kwa ajili ya kubaini changamoto zinazowakuta watoto wa kike katika kipindi cha hedhi wamebaini ukosefu wa elimu ambayo baadhi ya watu wamepata magonjwa yatokanayo na hedhi isiyo salama hivyo ameiomba serikali kutoa ushirikiano katika kumaliza tatizo hilo nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top