Rais Dkt John Pombe Magufuli leo amezindia awamu ya kwanza ya miuondombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) hafla iliyofanyika katika kituo cha mabasi hayo kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani.
Katika uzinduzi huo alihudhuria pia Makamu wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika na Mwakilishi wa Benki ya Dunia wa Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kutokana na mradi huo kujengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na Benki ya Dunia.
Serikali imeeleza mpango wake wa kujenga miundombinu ya mabasi ya mwendokasi ambapo mpango huo umegawanyika katika sehemu sita katika jiji la Dar es Salaam ikiwa ni njia ya kupungaza msongamano wa magari unaosababishara hasara kubwa kwa serikali na wakazi wa jiji hili.
Baada ya kuzindua mradi huo, Rais Dkt Magufuli aliendesha kidogo basi la mwendokasi akiashiri kuyazindua rasmi.
Mradi huo wa kipekee nchini Tanzania ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza foleni na watu kuweza kuwahi maeneno yao ya kazi na nyumbani ulianza kutumika mwezi Mei mwaka jana.
Post a Comment