Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Walichoafikiana Serikali na wenyeviti wa mitaa

Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na Wenyeviti wa Serikali za mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serikali za mitaa.

Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi kutoka serikali za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka hapo baadae itakapojadiliwa tena.

''Hakukuwa na dhamira yeyote ya kupunguza mamlaka ya heshima yenu Wenyeviti, lakini kama mihuri inaweza kupunguza heshima yenu nimeona kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili tene upya swala hili" amesema

Sanjari na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa kulikuwa na sababu za msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri kutokana na matumizi mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na kupelekea kuigawa ardhi bila utaratibu maalumu.

Hata hivyo Katibu wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam Mariam Machicha ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi kulifanyioa kazi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top