Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MKUU AFUTA POSHO ZA VITAFUNWA HALMASHAURI ZOTE NCHINI.



NI KUFUATIA OMBI LA KAIMU RC WA DAR ES SALAAM ALLY HAPI

NI ZILE ZILIZO NJE YA UTARATIBU WA KISHERIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amefuta posho zote ambazo hazipo kwa mujibu wa sheria, kwa watumishi na madiwani wa halmashauri zote nchini.

Miongoni mwa Posho zilizofutwa kuanzia mwezi huu, ni pamoja na posho ya vitafunwa, posho ya mazingira magumu ya kazi kwa wakuu wa idara, posho za kuchochea maendeleo na kujengewa uwezo zinazolipwa binafsi kwa madiwani na aina nyinginezo zote ambazo kisheria hazipaswi kuwepo na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha fedha hizo zinapelekwa kwenye miradi ya maendeleo.

Maamuzi hayo yametolewa leo jijini Dar es salaam wakati Waziri Mkuu alipokutana na watumishi wa manispaa ya Kigamboni, wakati alipofanya ziara ya siku moja kutembelea wilaya hiyo mpya mkoani humo.

Mh. Waziri Mkuu amefikia maamuzi hayo baada ya kuombwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ALLY HAPI kuangalia uwezekano wa kuzifuta posho ambazo hazipo kwenye utaratibu wa kisheria, na kuelezea kuwa halmashauri za mkoa wa Dar es salaam zilikuwa zinatenga na kulipa zaidi ya shilingi bilion 4.5 kwa mwaka kwa ajili ya posho za vitafunwa, mazingira magumu ya kazi, kujengewa uwezo n.k. fedha ambazo amependekeza zinaweza kusaidia kujenga madarasa zaidi ya 250 ya sekondari kwa mwaka mmoja ili kuziba upungufu wa vyumba vya madarasa na kuwapa nafasi wanafunzi waliofaulu na kukosa nafasi kupata elimu.

"Amesema hapa Kaimu Mkuu wa Mkoa Hapi, kuwa kuna utaratibu wa kulipana posho zilizo nje ya utaratibu wa kisheria kwenye manispaa...Naagiza kuanzia Januari hii posho hizo zisilipwe na nimezifuta rasmi. Mkurugenzi yeyote atakayelipa atakua amejiandalia mazingira ya kupoteza nafasi yake..."
Amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania KASSIM MAJALIWA pia amewataka watumishi wa umma nchini, kuwajibika kwa mujibu wa majukumu ya kazi zao na kuachana na utamaduni wa njoo kesho.
Kuhusiana na watumishi kumi waliohamishiwa kwenye halmashauri ya manispaa ya Kigamboni na kushindwa kuripoti, waziri mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi hao kufika vituo vyao vya kazi.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amemuomba waziri mkuu kushughulikia changamoto ya kimamlaka inayoikabili wilaya hiyo, kutokana na kuwepo Mamlaka ya Uendelezaji Mji wa Kigamboni KDA inayomiliki asilimia 12 ya ardhi, na Manispaa inayomiliki asilimia 88 ya ardhi yote.
Naye Mbunge wa Kigambon Dk Faustine Ndungulile, amemuomba waziri Mkuu kushughulikia changamoto zinazowakabili wakazi wa Kigamboni wanaotumia daraja la Nyerere, ambazo miongoni mwake ni foleni za magari na gharama kubwa ya tozo kwa mabasi ya abiria yanayotumia daraja hilo .
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top