Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AUDIO: Askofu Gwajima aeleza sakata zima la RC Makonda kutumia vyeti feki vya kielimu

Siku kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa hawezi kujibu madai ya mitandao ya kijamii kuwa alitumia vyeti vya mtu cha kidato cha nne, Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kusema kuwa ni kweli alitumia vyeti hivyo.

Askofu Gwajima amesema kuwa anamfahamu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite na kwamba hilo la Paul Makonda ni la mwenye vyeti hivyo.

Aidha, Askofu Gwajima amedai kuwa anavyovyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha kuwa hakufaulu na kwamba atashangaa kama Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako atalifumbia macho jambo hili. 

Pia ametishia kuwa, kama mamlaka husika hazitachukua hatua haraka basi yeye atatoka hadharani na vyeti hivyo.

Hapa chini ni sauti ya Askofu Gwajima akihubiri kanisani kwake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top