DAR ES SALAAM: HAKILA kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho wake, hatimaye mume wa ndoa wa nyota wa filamu Bongo, Kajala Masanja, Faraji Agustino yuko huru akidunda mtaani baada ya kutoka jela katika Magereza ya Keko jijini Dar na kusema ole wao waliokuwa wakichepuka na mkewe, Amani limenyetishwa
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka karibu na familia ya Faraji, alitoka jela siku kumi zilizopita baada ya kushinda rufaa ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya kudaiwa kutakatisha fedha haramu na kuuza nyumba iliyokuwa kwenye zuio.
KIKUBWA MTAANI
Hata hivyo, kutoka jela kwa mwanaume Mume wa Kajala kumeibua mambo mtaani kufuatia madai kwamba, hajaonana na mkewe kwa sababu ya wasiwasi juu ya nini kitatokea kufuatia maneno ya uchepukaji ya mkewe yaliyokuwa yakimfikia akiwa gerezani na mumewe huyo kusema atakwenda sambamba na wachepukaji wote.
Kajala na Mumewe
TUJIUNGE NA CHANZO
“Unajua ukweli ni kwamba, Kajala ni mke halali kabisa wa Faraji. Na akiwa jela, hata nyie Global (wachapishaji wa magazeti ya Amani, Uwazi, Wikienda, Ijumaa, Championi na Risasi) mliwahi kuandika habari kuhusu Kajala na mambo yake ya wanaume mtaani wakati mumewe akiwa gerezani.
“Sasa jamaa ametoka na amesema ole wenu mliochepuka na mke wangu. Lakini kikubwa ni kwamba, itakuwaje kuhusu ndoa yake?
Je, ndoa bado ipo au?
Je, mume alipotoka kafikia wapi?
Maana kwa vyovyote vile lazima alipofikia awe na mkewe ambaye ni Kajala,” kilisema chanzo hicho.
Kajala na Mchepuko wake Quick Laker
WALIOTEMBEA NA MKEWE
Chanzo hicho kikiongea huku kikisitiza kusitiriwa jina kwa kuhofia kuzodolewa kwa kutoboa siri za watu, kiliendelea kusema kuwa, taarifa zilizopo ni kwamba, baadhi ya wanaume waliowahi kubanjuka na Kajala sasa matumbo joto kwani wanaamini jamaa anaweza kuchukua hatua kali dhidi yao.
“Unajua ugoni?
Ugoni ni kumshika mtu akitembea na mkeo au mumeo. Sasa jamaa wale nasikia wanahofia kukutwa na hali hiyo kwani jamaa anaweza kwenda kuwashitaki kama ushahidi ni mkubwa,” kilisema chanzo hicho.
WALIOWAHI ‘KUTOKA’ NA KAJALA
Wanaume wanaotajwa ‘kutoka’ na Kajala baada ya mumewe kufungwa jela ni wasanii wa Bongo Fleva, Abott Charles ’Quick Roka’ na Msami Giovani ambaye iliwahi kuandikwa kuwa, alinunuliwa gari aina ya Toyota Fun Cargo na Kajala.
Wengine ambao waliwahi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kutoka na Kajala ni aliyewahi kuwa ‘jamaa’ wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, CK, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na msanii mwingine wa Bongo Fleva, Mutra.
MUME AONEKANA MAENEO YA LEADERS CLUB
Chanzo kikasema kuwa, tangu Faraji ametoka jela, amekuwa akikutana na washikaji zake kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Leaders Club, Kinondoni, Dar kwa ajili ya kubadilishana mawazo.
MUME AONEKANA MAENEO YA LEADERS CLUB
Chanzo kikasema kuwa, tangu Faraji ametoka jela, amekuwa akikutana na washikaji zake kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Leaders Club, Kinondoni, Dar kwa ajili ya kubadilishana mawazo.
Amani, juzi saa sita mchana lilifika kwenye baa hiyo na kukaa kwa muda wa saa tatu lakini bila kumwona ambapo mhudumu mmoja wa baa hiyo alisema katika sura anazoziona eneo hilo hakuna sura ngeni.
KAJALA AULIZWA YOTE
Kwanza ili kubaini ukweli wa Faraji kutoka gerezani, Amani juzi lilimtafuta Kajala mwenyewe ambapo alifunguka hivi: “Ni kweli mume wangu ametoka jela. Kwa kweli katika mambo ambayo namshukuru sana Mungu ni pamoja na hilo maana kule jela si kuzuri kabisa.” Amani: Vipi wewe, tangu mumeo ametoka umeonana naye mkaongea mawili matatu? Kajala: Hapana, hatujaonana bado. Amani: Vipi kuhusu ndoa yenu, mume ndiyo huyo katoka jela sasa, je unaizungumziaje ndoa? Kajala: Kwa sasa siwezi kusema lolote mpaka hapo baadaye ndiyo nitaweza kusema chochote.
KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mwaka 2013, Faraji alishitakiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) akidaiwa kutakatisha pesa haramu na kuuza nyumba iliyo kwenye zuio la kuuzwa kutoka kwa taasisi hiyo.
Kuuzwa kwa nyumba hiyo iliyopo Mbezi Beach, kunadaiwa ndiko kulikomwingiza Kajala kwenye kesi ambayo hukumu yake ilitoka kwa Kajala kufungwa miaka 5 jela au faini ya shilingi milioni 13 ambapo alilipa faini hiyo kwa kupewa nguvu na Wema Sepetu waliyekuwa wakiivana wakati wakati huo. Mumewe alihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela au faini ya shilingi milioni 200 ambazo alishindwa kuzilipa.
Hata hivyo, alikata rufaa ambayo ilisikilizwa na kutolewa hukumu mwaka jana ambapo alishinda lakini kesi ya kutakatisha pesa isiyokuwa na dhamana iliendelea mpaka alipoachiwa hivi karibuni.
Loading...
Post a Comment