Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ndoa ya Mbasha yavunjika .... Mahakama yagawa Mali .... Mpenzi mpya wa Flora aanikwa

Baada ya msuguano wa miezi kadhaa, hatimaye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imeridhia kuvunja ndoa ya Mwanamuziki wa Injili, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha kisha kugawana mali walizochuma pamoja. Chanzo makini kimefunguka kuwa, Flora aliyekuwa akiidai talaka hiyo ili aweze kuolewa na mwanaume wake mpya, alifanikiwa azma yake hiyo hivi karibuni baada ya mahakama kuridhia.

“Si unajua Flora ameshapata bwana mpya yule Daud Kusekwa na vikao nasikia vimepamba moto. Hivyo alikuwa anapambana kwelikweli kuhakikisha anapewa talaka na mimi ninayo nakala yake kama vipi niwatumie.

“Sasa amefanikiwa, wamegawana mali na mahakama imewapa masharti juu ya malezi ya mtoto wao aitwaye Eliza kwamba Flora ndiye atakayempa mahitaji yote ya msingi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Si unajua wale kuna mali walichuma pamoja? Basi zote wamezipiga pasu. Kuanzia zile zilizokuwa kwenya akaunti ya pamoja na hata ile nyumba yao iliyopo Tabata Kimanga.”

Risasi Jumamosi baada ya kuipata nakala ya hukumu hiyo ya talaka, lilimvutia waya Flora ili kumsikia anazungumziaje hatua hiyo lakini simu yake haikupatikana hewani.

Kwa upande wake Mbasha, alikiri ndoa yao kuvunjika mahakamani na kusema hayuko tayari kuzungumzia mgawanyo wa mali zao. “Wewe elewa tu tumeshaachana, talaka imetoka mahakamani.

Hayo mambo mengine mimi siwezi kuyazungumzia,” alisema Mbasha. Wawili hao kwa sasa kila mmoja ameshampata mwenzi. Flora anatarajia kuolewa Aprili 30, mwaka huu wakati Mbasha bado haijajulikana kama atamuoa mchumba wake wa sasa au la.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top