Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Bandarini .... Akutana tena na madudu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha vitu mbalimbali nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popot

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha vitu mbalimbali nje ya nchi.



Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari pamoja na vitu vilivyochakaa March 23,2017

Moja ya kontena likiwa lina gari ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza mitumba lakini kumbe ndani yake wanakuwa wameficha magari ya kifahari.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo.

Picha na lkulu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top