Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Chadema wageukia uchaguzi wa Kenya

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kumuunga mkono Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Msimamo huo umetolewa jana katika mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho unaofanyaki mjini Dodoma, ikiwa ni maamuzi ya Baraza hilo, na kutangazwa rasmi na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

Akizungumzia uamuzi huo, Mbowe alisema sababu kuu ya uamuzi huo ni kugeukwa na mgombea wa muungano wa ODM Raila Odinga, ambaye chama hicho kilikuwa kikimuunga mkono mara zote.

Mbowe amesema "Kwa muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono Raila Odinga achukue nafasi ya kuliongoza Taifa la Kenya. Mwaka 2015 ilipofika zamu yetu rafiki yetu Raila Odinga alitugeuka na kumuunga mkono adui yetu. Sisi kama Chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Umoja wa vyama vinavyounda JUBILEE".
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top