Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DC Mtaturu akabidhi nyumba 12 za Waalimu

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizindua rasmi nyumba zilizojengwa kwa ajili ya walimu wa shule za sekondari za  Minyughe na Wembere baadhi ya aliofuatana nao ni mwenyekiti wa CCM wilaya Hassan Tati mwenye shati la kijani na Diwani wa kata ya Minyughe Saddack.
 
               Jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 12  za walimu  ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua nyumba 12 za walimu  baada ya kuzindua.

 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na  viongozi wa wilaya,kata na walimu waliokabidhiwa nyumba  kwenye shule ya sekondari ya Minyughe
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akimpongeza mmoja wa walimu waliokabidhiwa nyumba ya kuishi kupitia mpango wa SADEP II wilayani humo.
..........................................................................................................................................
MKUU wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu amekabidhi  nyumba 12 za walimu wa shule ya Sekondari ya Minyughe na Wembere huku akiwaasa walimu kumpa nguvu rais dokta John Pombe  Magufuli  kwa kuzitunza ili zidumu na kama  sehemu ya kuunga mkono jitihada zake za kuwatumikia wananchi.

Nyumba hizo zimejengwa kupitia mpango wa serikali wa kuendeleza shule za sekondari(SEDEP II) uliogharimu shilingi milioni 300 hadi kukamilika kwake.

Akikabidhi nyumba hizo Mtaruru alimshukuru rais dokta  Magufuli kwa dhamira yake njema ya kuwahudumia watanzania ili wawe na maisha mazuri ikiwa ni utekelezaji  wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)ya mwaka 2015 iliyoeleza uboreshaji wa elimu ikiwemo mazingira ya kufundishia.

“Tukio hili ni ushahidi tosha wa namna ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo,nyumba hizi zitasaidia kuwasogeza walimu karibu na mazingira ya shule na hivyo kuwapa utulivu wa kuandaa masomo yao hali itakayosaidia kuongezeka kwa ufaulu kama moja ya maazimio ya mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika mwezi disemba mwaka jana  lakini pia itaondoa kero ya walimu kuhangaika mitaani,”alisema Mtaturu.

Aliwataka walimu kuendelea kuiamini serikali wakati inaendelea kushughulikia kero,stahili na madai yao na kuwapongeza  kwa ushirikiano walioutoa kwa wakandarasi  uliorahisisha mradi huo kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri Ally Mwanga alisema uamuzi wa kupeleka mradi huo kwenye shule hizo aliufanya kwa kushirikiana na madiwani baada ya kata hizo kuwa na mazingira magumu ya kukosekana hata nyumba za kupanga na kuwapongeza wataalam kwa kukamilisha ujenzi kwa wakati na kwa kiwango bora.

"Tunaishukuru serikali yetu kwa kuwajali walimu kwa kuhakikisha wanapata makazi bora lakini pamoja na upatikanaji wa nyumba hizi bado kuna uhaba wa makazi ya walimu ambapo mahitaji ni nyumba 524 na zilizopo ni 60 tu,”alisema Mwanga.

Mkuu wa shule ya Minyughe mwalimu Augustino Nkhotya akizungumza kwa niaba yaw engine alisema kukamilika kwa nyumba hizo ni ukombozi mkubwa kwa kuwa awali walikuwa na nyumba mbili hali iliyowalazimu walimu kupanga umbali wa zaidi ya kilomita mbili na hivyo kupunguza tija ya ufundishaji.

Naye, mwenyekiti wa CCM wilaya Hassan Tati  aliipongeza serikali kupitia mkuu wa wilaya kwa utekelezaji mzuri wa  ilani ya  CCM ambayo kipindi cha kampeni waliinadi  na wananchi waliichagua na kuahidi  kuendelea kutoa ushirikiano kwa  serikali na wananchi katika kuboresha maisha yao.

Mradi wa SEDEP II ulitengewa jumla ya shilingi milioni 777 kwa wilaya ya Ikungi ikiwa ni ujenzi wa madarasa,nyumba za walimu na matundu ya vyoo miradi ambayo yote imekamilika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top