Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Hawa wanatafutwa kwa mauaji Kibiti ...



JESHI la polisi mkoani Pwani ,limewabaini baadhi ya mtandao wa watuhumiwa wa mauaji yanayoendelea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji wapatao kumi na mbili akiwemo mwanzilishi wa mauaji Abdurshakur Ngande Makeo .

Aidha jeshi hilo linaendelea na msako kuwatafuta watu hao ambao wanne picha zao zimepatikana na Donge Nono litatolewa kwa atakayefanikisha Taarifa zitakasozaidia  kukamatwa kwao.

Akizungumzia hali ya kiusalama ya Mkoa kutokana na vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika wilaya hizo ,Kamanda wa polisi mkoani hapo,Onesmo Lyanga ,alisema wanaendelea na mapambano na upelelezi kuwapata wahusika wote .

Alieleza jeshi la polisi limewabaini kwa majina na picha kwa baadhi yao .

Kamanda Lyanga ,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Faraj Ismail Nangalava ,Anaf Rashid Kapera @Kapelo ,Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa .

Wengine ni Shaban Kinyangulia ,Haji Ulatule ,Ally Ulatule ,Hassan Uponda ,Rashid Salim Mtulula ,Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri  na Hassan Njame .

Kamanda Lyanga ,alieleza kwamba ,Saidi Ngunde inadaiwa anaishi Ikwiriri na Omar Abdallah Matimbwa anaishi Dar es salaam ambapo picha zao wanazo pamoja na ya Faraj na Anaf .

Alieleleza wengine nane bado picha zao hazijapatikana hadi sasa .

“Jeshi letu limebaini hayo kwa kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi ” alibainisha .

Kamanda Lyanga alisema ,watuhumiwa hao ,wamegundulika kuwa hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga ,kisiwa cha Saninga kijiji cha Nchinga .

Kamanda huyo ,alifafanua kijiji kingine ni cha Mfesini kata ya Nyamisati na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti ,Rufiji na Mkuranga.

Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa siri kufichua watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama kimkoa, Jeshi Limetangaza bingo ya kumpatia sh. mil .tano yeyote atakaefanikisha zoezi hilo .
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top