Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Hii hapa orodha ya Watu waliochaguliwa kujiunga na JKT Mei 2017



TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017.


Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za
  •  JKT Rwamkoma – Mara, 
  • JKT Msange – Tabora, 
  • JKT Ruvu – Pwani, 
  • JKT Makutopora – Dodoma,
  •  JKT Mafinga – Iringa, 
  • JKT Mlale – Ruvuma, 
  • JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga,
  •  JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, 
  • JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.


Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:

  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  2. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahariSoksi ndefu za rangi nyeusi.
  3. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  4. Track suit ya rangi ya kijani au blue
  5. .Nauli ya kwenda makambini na kurudi majumbani.
Mkuu wa JKT anawakaribisha Vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na Vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, Stadi za kazi, Stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Ilitolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 22 Mei 2017
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top