Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Matajiri walivyomiminika na magari ya kifahari kumzika Ivan

 UGANDA: WAKATI watu wengi walikuwa wakiomboleza kifo cha Ivan Semwanga, matajiri wakubwa na watu maarufu katika jiji la Kampala, waliitumia fursa hiyo kujitokeza na kuonyesha magari yao ya bei mbaya.

Wakati ibada ya mazishi ya Ssemwanga iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Paul la Namirembe mchana huu, matajiri wengi walijitokeza katika msururu mrefu ambao ulisababisha msongamano wa magari katika barabara ya Namirembe.

Pamoja na magari hayo kuwa ya bei kubwa, mengi yalikuwa na majina ya wamiliki wake badala ya namba za usajili na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa watu waliohudhuria mazishi hayo.

Matajiri maarufu kama Jack Pemba, Lwasa, Mugisha na  mwanamuziki  Bebe Cool, walikuwa miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria ibada hiyo.

Ivan Semwanga alifariki katika Hospitali ya Biko Academy nchini Afrika Kusini, Alhamisi wiki iliyopita kutokana na ugonjwa wa moyo na anazikwa leo nyumbani kwao Kayunga.



Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top