Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli afanya uamuzi mzito TBC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewasamehe wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa kosa la kurusha habari ya uongo kumhusu kiongozi huyo wa nchi.

Wafanyakazi hao walisamishwa kazi mwezi Machi kwa kuhusika katika makosa ya kiweledi na kiuhariri yaliyosababisha kutangazwa kwa taarifa ambayo haikuwa sahihi Machi 03, 2017.

Wafanyakazi hao walirusha hewani taarifa ya uongo iliyosambazwa na mtandao wa Fox Channel.com kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amesifu utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli na kwamba ni mfano mzuri wa kuigwa Afrika.

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba, ilieleza kuwa makosa hayo yalileta usumbufu kwa umma na yasingefanyika endapo taratibu zote za kitaalamu zingefuatwa kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe.

Watangazaji waliotangaziwa msahama huo ni Rais Dkt Magufu ni pamoja na Gabriel Zackaria, Elizabeth Mramba, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai. 

Rais Dkt Magufuli alitoa msamaha huo alipofanya ziara katika kituo hicho jana ili kuangalia utendaji kazi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi kuweza kutambua changamoto zinazowakabili.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top