Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali kusambaza mifuko maalum ya kujifungulia kwa Wanawake nchini

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa inategemea kusambaza  vifuko maalum vya kujifungulia vyenye vifaa vya kujifungulia  kwa wanawake  500,000 ambavyo vitasambazwa nchi nzima kulingana na uhitaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhe.Dk Khamis Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Munira Mustafa Khatibu leo Bungeni Mjini Dodoma.

“Sera ya Afya ya mwaka 2007 inaeleza kuwa Huduma za kina Mama wajawazito katika vituo vya ngazi zote zinapaswa kutolewa bila malipo”,Alisisitiza Mhe.Kigwangala.Aidha amesema kuwa Serikali haijawahi kuweka tozo na gharama za vifaa vya kujifungulia na upasuaji na hivyo huduma hizo zitaendelea kutolewa katika ngazi zote katika vituo vya umma vya kutolea huduma kwa gharama za Serikali.

Aidha kwa upande mwingine Mhe,Kigwangala ametoa rai kwa Wabunge kusaidia  kusimamia utekelezaji wa Sera walizokubaliana katika katika maeneo yao husika ili kuhakikisha huduma hizi za kina mama zinapatikana kwa Gharama za Serikali kama ilivyopangwa.

“Ili azma ya Serikali ya Kuhakikisha akina mama wajawazito wanapata huduma nzuri na lengo la kupunguza vifo vya mama na watoto inafanikiwa ni lazima usimamizi uwe wa karibu sana”,Aliongeza Mhe.Kigwangalla.
Aidha jumla ya kina mama 1,900,000 hujifungua kila mwaka nchini na kumekuwa na changamoto katika upatikanaji wa vifaa ambapo kwa sasa Serikali imeliwekea mkazo suala hilo ili kuhakikisha kina mama hao wanajifungua salama.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top