Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Viongozi mbalimbali wafunguka mazito juu ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini

Dar es Salaam. Baadhi ya wabunge wameibua hoja tofauti kwenye mitandao ya kijamii baada ya Rais John Magufuli kupokea ripoti ya mchanga wa madini Ikulu, leo.

Katika akaunti yake ya Twitter, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameandika, “pongezi kwa kazi nzuri iliyofanywa na tume.”

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa Twitter ameandika, “utafiti unapingwa kwa utafiti. Kwa sasa Kamati ya Mruma Ndio rejea sahihi kwenye suala la mchanga na hivyo nakubali mapendekezo yaliyomo.”

Naye, Naibu Waziri Afya, Hamis Kigwangalla katika akaunti yake yaTwitter ameandika, “sishangai kumsikia Rais wetu akisema 'wasomi' tumeiangusha nchi. Kwa kila namna tunapaswa kujitazama sana.”

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameandika, “nimemsikiliza mheshimiwa Rais na kuendelea kuielewa nia yake njema ya kuisaidia nchi yake. Tuko pamoja na ninakuunga mkono.”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top