Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM: Mali zote za Mafisadi kutaifishwa

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali mstaafu Ngemela Lubinga (pichani) amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imepania kutenda haki na kuzirudisha mali zote zilizoibwa na wabadhirifu.

Aliyasema hayo jana wakati akitoa mada kwenye darasa la itikadi kwa ajili ya vijana wa vyuo vikuu vya Mkoa wa Dodoma linalofanyika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo. Alisema Chama Cha Mapinduzi kimejipanga kuhakikisha mali zilizoibwa na wabadhirifu zinarudishwa na kusisitiza serikali itatenda haki wakati wa kutekeleza agizo hilo.

“Kila aliyetenda uovu na kuiba mali za umma atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Lubinga na kuongeza kuwa, hakuna fisadi wala mla rushwa atakayepona. “Serikali ya CCM imedhamiria kuzirudisha mali zote zilizoibwa, hakuna mtu atakayepona katika hili, lakini tutatenda haki,” alifafanua.

Alisema katika mapambano yanayoendelea hakuna fisadi, mla rushwa aliyetenda maovu ambaye atapona na kwamba wote watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Alishangazwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya Watanzania huku wengine wakiwa ni wale walioshika nyadhifa za juu katika nchi kwa kudai kuwa kudai nchi haina dira.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top