Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kaburi la Ivan wa Zari kufukuliwaHatimaye Mahakama Kuu ya Uganda yatoa amri kaburi la Ivan Ssemwanga, yule mtalaka wa Zari, ambaye ni mke wa sasa Diakond Platinumz lifukuliwe, ili mamilioni ya pesa alizozikwa nazo zitolewe.

Mahakama imesema imechukua uamuzi huo ili kulinda heshima ya fedha ya nchi hiyo.

Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya Mganda mmoja aitwaye Mgugu Abey, kuwashtaki Mahakamani  kampuni iliyoraribu mazishi hayo ya A Plus Funeral Management na Benki Kuu ya Uganda,ambayo imeonekana ilizembea kwenye tukio hilo.

Hivyo, mahakama imeamuru kampuni ivunje kaburi kwa gharama zao,ili mlalamikaji achukue pesa hizo kwa niaba ya mataifa yenye fedha hizo, kwani zilikuwepo Rand za Afrika Kusini,Dola za Marekani pamoja na Shilingi za Uganda.

Kisha kampuni ya A Plus imeamriwa ilifukie kaburi hilo kwa gharama zake  na kisha kumlipa ndugu Abey gharama zingine za usumbufu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top