Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAGUFULI NI MAKTOUM WA TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Mhe Antony Mtaka (Picha Na Mathias Canal)
Mwandishi ni ANTHONY MTAKA
Makala hii inapatikana Katika gazeti la Raia Mwema la tarehe 08.06.2017
KITABU cha *My Vision* (Dira Yangu) kilichoandikwa na mtawala wa Dubai, Sheikh Mohamed Bin Rashid Ali Maktoum kinaeleza wazi kwamba mabadiliko yoyote ya kiuchumi  kwa nchi  zinazokua,  kamwe hayawezi kuja kwa bahati mbaya.
Katika dhamira yake, Maktoum anasema amejizatiti na kuhakikisha anaweka malengo madhubuti  ya kufikia hadhi na malengo  ya uchumi  kimataifa na kuiona  Dubai inakua kwa haraka.
Anasema dira yake  ni kali, malengo yao  yapo wazi na matarajio yake ni imara katika kusimama adhima na changamoto zinazowakabili ili kusimamia dhima ya nchi yake na  kuwa ya kimataifa katika sekta zote.
Maktoum anafananisha mapinduzi ya kiuchumi sawa na mbio za simba na chui, ambapo anaeleza kuwa maendeleo yoyote hayaji kwa bahati mbaya, hivyo  kushindwa  kwa jambo si kuanguka na badala yeke yahitaji dhamira ya dhati katika kufanya mapinduzi.
Anasema kwenye kitabu chake kwamba kiongozi mwenye maono lazima asimamie maono yake kwa kujiamini tena bila woga wowote  ili kufikia malengo aliyojiwekea.
Anatoa ujumbe wa matumaini kwamba kama jamii yoyote itajiunga pamoja na kujiwekea malengo ya kufanikiwa katika nyanja mbalimbali, jamii hiyo, bila kujali tofauti zake za ndani, itapiga hatua kubwa kuelekea mafankio.
Licha ya kitabu hicho kueleza mambo mengi, zipo nukuu nyingine mbalimbali zinazoeleza malengo na matarajio ya viongozi majasiri ikiwamo, nukuu ya kitabu cha Waziri Mkuu wa sasa wa India, Narendra Modi.
Katika Kitabu hicho: The Modi Effect, kilichoandikwa Lance Price, ananuku sehemu ya hotuba ya Waziri Mkuu huyo wa India katika wakati wa uapisho wake,
Sehemu ya nukuu hiyo inasema; “I can see before my eyes Mother India Awakening Once Again, nukuu hiyo ya Modi ina ujumbe sawa na maneno ya Rais Dk. John Magufuli anaposema; “Nataka Tanzania mpya”. Na hakika, kwa haya anayofanya Dk. Magufuli  ni dhahiri Mama Tanzania atasimama tena.
Aidha, tangu  achaguliwe Dk. Magufuli ameweza kujipambanua katika  dhamira yake ya dhati ambapo wakati wa kampeni  zake mwaka  2015, aliweza kujinadi vilivyo  na kuitangaza ilani ya Chama chake  cha Mapinduzi katika mlengo wa kuibadili Tanzania.
Hata hivyo, kama ilivyo ada ya binadamu wapo  waliomuelewa na ambao hawakumuelewa wakati anajinadi na kutoa ahadi zake kwa wananchi  na wengi  wao walidhani ni masuala  ya kisiasa kutokana na viongozi waliopita  kuwa wakitoa ahadi nyingi, lakini wakishindwa kuzitekeleza.
Kwake imekuwa  tofauti. Katika kipindi cha miaka miwili kuwa  madarakani ameweza kufanya mambo makubwa  kwa kusimamia dira mipango na dhamira yake ya dhati na   kuona matokeo chanya ya  utendaji wake wa kazi .
Ni  kipindi kifupi cha uongozi  wake ambao umeweza kumfananisha na mtawala wa Dubai Sheikh Mohamed Bin Rashid Ali Maktoum   na baadhi ya viongozi wengine wachache waliopigania mapinduzi ya uchumi wa nchi zao kama Waziri mkuu wa India Narendra Modi, na Rais Paul Kagame wa Rwanda.  
Naweza kusema kuwa kuna utofauti kwa viongozi wenzake waliopita mbali  na mazuri waliyoyafanya. Yeye ameweza kuutafuna mfupa ndani na nje ya Bunge wakati wa  mapendekezo aliyowahi  kuyatoa katika sekta mbalimbali ili  kukuza  uchumi wa nchi.
Uongozi wake tayari umeweza kufanya mambo makubwa sana na kuirudisha Tanzania katika njia na mstari ulionyooka kwa kuitangaza  Tanzania na  kuwa ni filimbi  nchi zingine kuiga mfano wa uongozi mzuri na madhubuti wa Rais Magufuli.
Jambo la kujivunia na la kumpongeza  Rais Magifuli kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake  limenifanya  kuona viashiria vya maendeleo ya kasi kutoka kwa  kiongozi  wetu mahiri na shujaa ambaye anataka Tanzania iamke itoke ilipo na kuwa na taswira nyingine ya uchumi na viwanda.
Katika kulithibitisha hilo Rais Magufuli ameweza kufufua Shirika la Ndege, Shirika la Reli, kafanya mapinduzi ya Bandari, kakuza uchumi wa Tanzania, kajenga picha na taswira mpya ya Utumishi wa Umma ikiwa ni sambamba na mrejesho wa haraka wa nidhamu kwa watumishi wa umma.
Aidha, katika kulinda na kusimamia rasilimali za Taifa lazima Watanzania wakubali kuimba wimbo mmoja na Rais , kuwa na mbiu ya mgambo kama zilivyokuwa enzi za harakati za Mwalimu Julius Nyerere ambapo hata  mataifa mengi yaliyokuwa vizuri kiuchumi  yalifanya  maamuzi magumu.
Sambamba na kufanya mambo makubwa kwa manufaa ya nchi, pia itoshe kusema kuwa hotuba ya Rais Magufuli ya mwezi Machi  24, mwaka huu  iliyogusa sekta ya madini itabaki kuwa ya kukumbukwa na Watanzania. Ni siku ambayo Rais Magufuli aliiambia dunia na Tanzania kuwa yupo kamili na tayari kwenda kwenye dhamira ya uchumi wa kati na  kuwa nchi wafadhili.
Hotuba hiyo imepokewa na Watanzania kuwa kama  mithiri ya timu ya Taifa iliyopata medali ya dhahabu  katika suala la makinikia.
Nampongeza sana Rais kwa kutoa uongozi na kutoyumba katika dhamira yake hadi kutegua na kubaini  kitendawili cha makinikia ambacho hakikuteguliwa tokea miaka 17 iliyopita.
Matokeo ya tume zote alizounda yanaimarisha hoja na sababu ya kurudi mezani kujadili upya mikataba ya madini ambayo iliwekwa toka hapo awali.
Lakini pia matokeo ya tume hizo yanatupa mafunzo mengi ikiwa tutayaangalia kama muendelezo, na tulipokuwa  na uchimbaji  mkubwa wa madini hatukuwa na uwezo wa kuhakiki madini na tulitegemea kampuni ya Alex Sterwart ya nje na tutagundua  kuwa hatuna uhakika ikiwa tulichoambiwa ndicho sahihi ama tumepunjwa.
Kwa kazi nzuri anayoifanya Rais, tumuunge mkono kwa hatua alizochukua  za kuwapumzisha Waziri wa Nishati na Madini , Bodi ya TMAA, Mkurugenzi na Menejimenti  kutokana na taarifa hii, na ni muhimu kwao kuwajibika kisiasa  kwa kuwa kwa vyovyote vile matokeo ya tume yamewaondolea imani mbele ya macho ya Watanzania.
Aidha,  matokeo ya tume ya awali  yamejibu kitu tulichojua na kuamini kutoka sekta ya madini nchini ambayo yameleta taharuki ndani na nje ya nchi kati ya serikali na wawekezaji  wa makampuni ya madini , kati ya bodi na wahisani katika makampuni ya madini na pengine kati ya nchi na nchi.
Jambo moja ni dhahiri, kwamba katika suala hili la makinikia baadhi ya wasomi wetu walishindwa kutumia uzalendo wao wa kuiendeleza nchi kwa kutoa utaalamu wao katika sekta mbalimbali.
Wakati umefika kwa Bunge kupitia upya sheria na mikataba ya madini ili kubaini ukakasi upo wapi ili marekebisho yaweze kufanyika na kuendana na kasi hii ya ujenzi wa Tanzania mpya katika ulinzi wa rasilimali zetu.
Lakini si Bunge tu. Hata vyama vya wanasheria, watu binafsi, makundi na vyama mbalimbali vya waandishi wa habari, vyuo vikuu na vyuo vingine, viingine katika kazi ya kupambania maslahi ya Tanzania kwa kuanzia na suala hili la makinikia.
Kwenda mbele, pengine sasa tuone haja  ya kuweka mfumo utakaowezesha taasisi zinazoshughulikia vitu nyeti kama madini (TMAA), ziwe zinatoa kwa uwazi taarifa zao za kila mwaka kama ambavyo inafanya ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na taarifa hizo ziwe zinajadiliwa na Bunge.
Antony Mtaka ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu* na *Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (0657 995 131)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top