Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwigulu Nchemba ajenga hostel 22 kwa shule zote jimboni mwake

Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ameanzisha Ujenzi wa hostel za kike 22 katika shule za sekondari 22 zilizopo katika kata 20 ndani ya jimbo lake la iramba.
Mradi huu mkubwa wa kukuza elimu jimboni hasa kwa wasichana ambao wanakutana na vikwazo vingi unafanywa kati ya ofisi ya Mbunge na wananchi wa jimbo hilo na ukikamilika utasaidia asilimia zaidi ya 70 ya wanafunzi wa kike kwenye jimbo hilo.
Mbunge mpaka sasa amesaidia kila kata mifuko 100 na nondo za kutosha za ujenzi huo huku wananchi wakitoa matofali na mafundi wa kujenga hostel hizo na ujenzi ushaanza kwa kata zote na upo katika hatua nzuri.
"Nimeukagua mradi katika shule ya kizaga iliyopo kata ya ulemo nimefurahishwa na wananchi walivyojitoa nitaleta mifuko 100 ya cement kukamilisha hostel hii na kupaua tumepata mfadhili atamaliza kila kitu mpaka kukamilika kwake na kuanza kutumika. Ikikamilika itachukua na wanafunzi wa kike zaidi ya 160 wakati shule inawanafunzi wakike 180" --Waziri Mwigulu
Mpango wetu ifikapo mwezi December mwaka huu ziwezimekamilika hostel zote 22 katika kata 20.
Imetolewa Na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Iramba Magharibi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top