Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli atoa hekari 65 za Magereza na kuwagawia Wananchi

Rais John Magufuli amewapa wakazi wa Bagamoyo, eneo la Magereza lenye ukubwa wa heka 65.

 Rais Magufuli amechukua uamuzi huo leo (Alhamisi) wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.

Alichukua hatua hiyo baada ya wanawake waliokuwa wamebeba mabango, kumtaka awape eneo lao kwa kuwa ni wazaliwa wa Bagamoyo, ni wajane na wana uhaba wa maeneo ya biashara.

“Akina mama mnaokaa huko na akina baba nimewapa hilo eneo lakini natoa tahadhari, mpaka wenu sasa ni barabara, msivuke mkaenda upande ule,” amesema.

Amelitaka Jeshi la Magereza kufanya mabadiliko katika hati ili eneo hilo liwe la wananchi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top