Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ratiba ya Mazishi ya Mzee Ndesamburo yatajwa

Moshi. Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo aliyefariki dunia jana atazikwa Jumanne ijayo.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa ameliambia gazeti hili kuwa Ndesamburo atazikwa katika makaburi ya familia nyumbani kwake eneo la Mbokomu.

Golugwa amesema Jumatatu, Juni 5 kwenye viwanja vya mashujaa mjini Moshi wananchi watapata fursa ya kuaga mwili wa Ndesamburo.

Katibu huyo amesema wakati wa kuaga mwili wake kutakuwa na salamu kutoka kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini na wawakilishi wa makundi mbalimbali.

Golugwa amesema msiba wa Ndesamburo umewagusa wengi nchini kutokana na mchango wake katika kukuza misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuchangia ustawi wa sekta ya utalii.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top