Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kibano kipya cha Wakurugenzi wa Halmashauri chaja

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, SELEMANI JAFO.

SERIKALI inakusudia kupeleka bungeni marekebisho ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa itakayowabana wakurugenzi wa halmashauri kurejesha asilimia 20 ya mapato kwa vijiji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, alisema jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini (CCM), Flateri Massay.

Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwalipa posho au mishahara wenyeviti wa vijiji na vitongoji ili kurahisisha ufanisi wa shughuli zao.

Akijibu swali hilo, Jafo alisema sheria hiyo itakuwa mwarobaini kwa wakurugenzi ambao wamekuwa hawarejeshi fedha hizo ambazo hutumika pia kuwalipa posho viongozi hao.

"Hii sheria sasa itawalazimisha wakurugenzi kurejesha hizo fedha ili kuwanufaisha walengwa na itaweka utaratibu mzuri wa kuzirejesha," alisema.

Aidha alisema serikali imeimarisha mifumo ya makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri zote ili kujenga uwezo wa kutenga asilimia 20 kwenda kwenye vijiji.

Alisisitiza kuwa serikali inathamini na kutambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na wenyeviti wa vijiji na mitaa katika maendeleo ya taifa.

"Serikali imezingatia na kuweka utaratibu wa kuhakikisha viongozi hao wanalipwa posho maalum kama motisha kupitia asilimia 20 ya mapato yanarejeshwa na halmashauri kwenye vijiji,"alisema

Alibainisha asilimia 17 ya fedha hizo zinatakiwa kutumika kwa shughuli za utawala ikiwamo kulipa posho ya viongozi hao na asilimia tatu kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top