Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali kuwapa vijana 3400 ujuzi wa stadi za maisha

UZINDUZI- IRINGA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Mhe Jenista Mhagama amezindua Programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi wa stadi za maisha ya Taifa kwa vijana, Mkoani Iringa mpango ambao utawanufaisha vijana elfu tatu mianne 3,400 mpango  unaogharamiwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli.

Mhe Mhagama amesema mpango huu ni sehemu ya kuwaandaa vijana ambao watashiriki katika mapinduzi ya viwanda nchi Tanzania na utasaidia kutoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa kupitia mafunzo ya Uanagenzi, katika nyanja za ujenzi, tehama, ufundi magari, na ushonaji nguo katika mikoa yote nchini Tanzania.

Katika awamu hii ya kwanza, mpango huu unaendeshwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania na taasisi ya Wasalesiani wa Don Bosco Tanzania.

Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Naibu waziri Mhe Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza, Wabunge kutoka mkoa wa Iringa, na Njombe na Mkuu wa Shirika la Wasalesiani wa Don Bosco Africa Mashariki Fr. Simon Asira.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top